Mjane akiwa na jirani yake nnje ya kibada chake
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Jerumana
Nyinge [50] mkazi wa kitongoji cha Usafwani kijiji cha Kongolo Mswiswi Kata ya
Mswiswi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amedhurumiwa nyumba na serikali ya
kijiji hicho.
Hii imekuja baada ya Mwanamke huyo kutelekezwa
kwenye kibanda cha nyasi kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu nyumba yake ya
bati ibomolewe ili kupisha shughuli za kimaendeleo kijijini hapo kwa ahadi
kwamba angeweza kujengewa nyumba nyingine ya kuweza kuishi.
Mjane huyo ambaye hana watoto amejikuta akiishi
kwa dhiki kwa kipindi chote cha masika ambapo baadhi ya vitu vimeharibika
kwa kunyeshewa na mvua kikiwemo chakula pamoja na kukosa mahali pa kulala
“Mume wangu alifariki mwaka 2007 na
kuanzia mwaka 2010 serikali ya kijiji imenihamisha na kunileta hapa
bila huduma za msingi kama maliwato na bafu ambapo nimekuwa
nikijisetiri kwa majirani na mara kadhaa wamekuwa wakinifukuza “ alisema
mjane huyo.
Kwa upande wake jirani wa mjane huyo
Bwana Mbwiga Mwayila amesema kuwa mjane huyo amekuwa akiishi maisha
hatarishi kutokana na umbali mrefu anaotembea kufuata huduma ya maliwato na
hasa nyakati za usiku amekuwa akiwagongea kuomba msaada huo na kuwa adha
kwao kwa kuwakatisha usingizi .
Bi Salome Mwampashi ni jarani wa
mjane huyo ambaye ameiomba serikali ya kijiji kumsaidia haraka mjane huyo ili
kuepuka usumbufu kwa majirani huku akisema ameshuhudia mama huyo
akipata taabu ya kupika wakati wa mvua kutokana na nyumba anayoishi kuvuja na
moto kuzimika
Naye mwenyekiti wa kijiji hicho
ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mswiswi bwa Fulugence Mhegele
amekiri kubomolewa kwa nyumba ya mjane huyo ilikupisha ujenzi wa maduka na kuleta
maendeleo ya kijiji ambapo amefafanua hapakuwa na mapatano ya kulipa
fidia ingawa diwani huyo hakuonesha mhutasari wowote wa makubaliano hayo
.
Na Ezekiel Kamanga Mbarali
Kwa yeyote yule aliyeguswa kumsaidia mjane huyu
piga simu namba hizi Ezekiel Kamanga 0754 49 07 52
joseph Mwaisango 0754 37 44 08
|
2 comments:
Hi thеre! Dο you know іf thеy make any plugins to
assіst wіth Ѕearсh Enginе
Оptimizаtiοn? I'm trying to get my blog to rank for some targeted keywords but I'm not seeing ѵеrу gοod gainѕ.
Ιf you know of any plеаse shaгe.
Apprесiate it!
mу hοmepage - Chill out
My webpage > just click the up coming page
Hii ni kuvunja khaki za binadam, huyo kiongozi wa kijiji achukuliwe hatua za haraka, huu ni udikteta mkubwa, utamuharibiaje mali raia na kumnyima khaki yake, ingekua ni yeye huyo kiongozi akafanyiwa hivi na serikali yake' angeona sawa, sasa hiyo serikali ya kijiji imemuamisha bila hata kumtimizia mahitaji yake mihimu, huyu mwanadam. Sasa ilikua inafikira nini? Akajisaidie wapi? Haya mambo ya utawala wa mabavu kama udikteta. Yanaudhi sana. Yamejaa, uoneaji, nadhuluma tu kwa watu masikini,
Post a Comment