Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, February 15, 2013

MJANE ADHURUMIWA NYUMBA NA SERIKALI YA KIJIJI


Mjane Jerumana Nyinge 50 akiwa ndani ya kibanda chake alichotelekezwa na serikali ya kijiji
Hapo ndipo anapolala mjane huyo
Hivi ndiyo vyombo anavyotumia kupikia mjane huyo
Hiki ndicho kibanda alichopewa na serikali ya kijiji hii ni sura ya mbele ya kibanda hicho
Hii ni sura ya nyuma ya kibanda hicho
Humu ni ndani ya kibanda hicho kuna tundu kubwa kwenye paa la manyasi mvua ikinyesha mjane huyo hawezi kulala maana maji yote huingia ndani
Hakika mjane huyu anaitaji msaada angala nae apate bati choo godoro la kulalia na mahitaji mengine ya kibinadamu tunaomba tusaidiane kumsaidia mjane huyu
Mjane akiwa na jirani yake nnje ya kibada chake


Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Jerumana Nyinge [50] mkazi wa kitongoji cha Usafwani kijiji cha Kongolo Mswiswi Kata ya Mswiswi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amedhurumiwa nyumba na serikali ya kijiji hicho.
Hii imekuja baada ya Mwanamke huyo kutelekezwa kwenye kibanda cha nyasi kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu nyumba yake ya bati ibomolewe ili kupisha shughuli za kimaendeleo kijijini hapo kwa ahadi kwamba angeweza kujengewa nyumba nyingine  ya kuweza kuishi.

Mjane huyo ambaye hana watoto amejikuta akiishi kwa dhiki kwa kipindi chote cha masika  ambapo baadhi ya vitu vimeharibika kwa kunyeshewa na mvua kikiwemo chakula pamoja na kukosa mahali pa kulala 


 “Mume wangu alifariki mwaka 2007 na  kuanzia mwaka 2010  serikali ya kijiji imenihamisha  na kunileta hapa bila huduma  za msingi  kama maliwato na bafu ambapo nimekuwa nikijisetiri kwa majirani  na mara kadhaa wamekuwa wakinifukuza “ alisema mjane huyo.

 Kwa upande wake jirani wa mjane huyo  Bwana Mbwiga Mwayila amesema  kuwa mjane huyo amekuwa akiishi maisha hatarishi kutokana na umbali mrefu anaotembea kufuata huduma ya maliwato na hasa nyakati za usiku amekuwa akiwagongea kuomba msaada huo na kuwa  adha kwao kwa kuwakatisha usingizi .

 Bi  Salome Mwampashi ni jarani wa mjane huyo ambaye ameiomba serikali ya kijiji kumsaidia haraka mjane huyo ili kuepuka usumbufu kwa majirani huku akisema  ameshuhudia  mama huyo akipata taabu ya kupika wakati wa mvua kutokana na nyumba anayoishi kuvuja na moto kuzimika 


 Naye  mwenyekiti wa kijiji  hicho ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mswiswi bwa  Fulugence  Mhegele amekiri kubomolewa kwa nyumba ya mjane huyo ilikupisha ujenzi wa maduka na kuleta maendeleo ya kijiji  ambapo amefafanua hapakuwa na mapatano ya kulipa fidia  ingawa diwani huyo hakuonesha mhutasari wowote wa makubaliano hayo .

Na  Ezekiel Kamanga Mbarali

Kwa yeyote yule aliyeguswa kumsaidia mjane huyu  

piga simu namba hizi  Ezekiel Kamanga 0754 49 07 52

                                       joseph Mwaisango 0754 37 44 08

2 comments:

Anonymous said...

Hi thеre! Dο you know іf thеy make any plugins to
assіst wіth Ѕearсh Enginе
Оptimizаtiοn? I'm trying to get my blog to rank for some targeted keywords but I'm not seeing ѵеrу gοod gainѕ.
Ιf you know of any plеаse shaгe.
Apprесiate it!

mу hοmepage - Chill out
My webpage > just click the up coming page

Anonymous said...

Hii ni kuvunja khaki za binadam, huyo kiongozi wa kijiji achukuliwe hatua za haraka, huu ni udikteta mkubwa, utamuharibiaje mali raia na kumnyima khaki yake, ingekua ni yeye huyo kiongozi akafanyiwa hivi na serikali yake' angeona sawa, sasa hiyo serikali ya kijiji imemuamisha bila hata kumtimizia mahitaji yake mihimu, huyu mwanadam. Sasa ilikua inafikira nini? Akajisaidie wapi? Haya mambo ya utawala wa mabavu kama udikteta. Yanaudhi sana. Yamejaa, uoneaji, nadhuluma tu kwa watu masikini,