Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, December 2, 2011

UCHAWI UCHAWI UCHAWI

MWANAMKE huyu ambaye hakufahamika jina lake amekutwa katika mazingra haya jana alfajiri maeneo ya Ilomba Jijini Mbeya akiwa kama alivyozaliwa, Inadaiwa kuwa mwanamke huyu ni mmoja wa wanafunzi wa chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU).

Wananchi walikusanyika katika eneo alipokutwa mwanamama huyu ambapo inadaiwa kuwa alikuwa akiwaqnga nyakati za usiku lakini akakutana na wababe wa Ulozi mitaa hiyo ndipo aliposhindwa kuendelea na ulozi wake na kujikuta akikosa nguvu na kushindwa kuendelea na safari yake ya ulozi hadi alipokutwa asubuhi kweupee!!!

Inaelezwa kuwa eneo hilo ni maarufu kwa kukamata watu wanaoingia anga hizo kwa ajili ya kufanya ugagula ambapo miezi michache iliyopita mtoto mdogo wa kike naye alibambwa akitaka kufanya ulozi na kukutwa na umati wa watu kabla ya kufanya ulozi wake.

Mwanamke huyu aliokolewa na askari polisi ambao walimchukua moja kwa moja hadi kituoni kwa ajili ya kuhifadhiwa ili asipate madhara zaidi.Jitihada za kukutana na uongozi wa chuo kikuu cha TEKU zinaendelea ili kujua kama mwanamke huyu alikuwa ni mwanafunzi wa chuo hicho kama inavyoelezwa na watu ama la.

Picha kwa msaada wa FACEBOOK ya Stanslaus Lambat na fasihi za ufasaha


8 comments:

G.Mwasambili said...

inawezekana ni mwehu mumemhoji?

Mbele said...

Hata mimi nilikuwa na wazo hilo hilo, ndugu Mwasambili. Tunawajibika kuwa wadadisi na kuangalia uwezekano wa aina mbali mbali. Je, pengine alilewa au kueleweshwa madawa ya kulevya? Pengine ameachwa hapo na wabakaji. Tukisema tu ni mchawi, bila uchunguzi zaidi, tunaweza kukosea.

Anonymous said...

Duh, mwanafunzi wa chuo kikuu mwehu?

Anonymous said...

Wabongo tunapenda kufikia uamuzi kwa kuendekeza dhana zetu tu. Zipi sababu hata 100 kidogo kwa huyu mwanamke kuwa hivi, lakini kwa sababu ya kutokuwa na elimu ya kutosha bado tumebaki na mambo ya kizamani kwamba kila kitu kisichokuwa na ufafanuzi wa wazi kinatokana na uchawi.

Anonymous said...

jamani mpeleke kwa dr.manyaunyau

Anonymous said...

Da mbeya imenichosha kwa matukio.du huu maji noma hapo mi no comment

mwallongo govarid said...

mbeya nyinyi noma

Anonymous said...

Napo sihami mbeya