Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, May 29, 2012

MADIWANI ILEJE WAMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI BI. SYLIVIA SIRIWA

MKURUGENZI MTENDAJI WA ILEJE BI.SIRIWA AKIWAOMBA RADHI MADIWANI KWAMBA HATA RUDIA TENA MAKOSA YA KIUTENDAJI

Pichani Bi Siriwa katikati akiwa ameshika tama baada ya madiwani kumsimamisha kazi) kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Ileje Mohamed Mwala) cheki zaidi

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA ILEJE BW. MOHAMED MWALA(mwenye joho jekundu) AKISISITIZA JAMBO KATIKA KIKAO KILICHOKETI KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ileje wamemsimamisha kazi Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi. Sylivia Siriwa kwa madai ya kuhusika na hujuma na ubadhirifu wa mali za halmashauri hiyo.

Hatua hiyo imefuatia tuhuma zilizoelekezwa kwake katika kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi kujadili jaribio la wizi wa fedha za halmashauri zilizofanywa na watumishi wanne ambapo Mkurugenzi huyo alishindwa kuwachukulia hatua za kisheria.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ileje Bw. Mohamed Mwala amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Baraza kujigeuza kamati ambapo Mkurugenzi alionekana kuhusika na makosa kwa kuwakumbatia watendaji hali ambayo imesababisha kutokuwa na imani naye



Habari kwa hisani ya Rashid Mkwinda



1 comment:

Anonymous said...

Mtafukuza wangapi? je,nyie madiwani kazi
mnaweza? mbona katani kwenu matatizo-
tupu? mi nadhani madiwani hawa wametu
mwa ,fukuzeni hata walimu walevi basi!