MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA ILEJE BW. MOHAMED MWALA(mwenye joho jekundu) AKISISITIZA JAMBO KATIKA KIKAO KILICHOKETI KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ileje wamemsimamisha kazi Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi. Sylivia Siriwa kwa madai ya kuhusika na hujuma na ubadhirifu wa mali za halmashauri hiyo.
Hatua hiyo imefuatia tuhuma zilizoelekezwa kwake katika kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi kujadili jaribio la wizi wa fedha za halmashauri zilizofanywa na watumishi wanne ambapo Mkurugenzi huyo alishindwa kuwachukulia hatua za kisheria.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ileje Bw. Mohamed Mwala amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Baraza kujigeuza kamati ambapo Mkurugenzi alionekana kuhusika na makosa kwa kuwakumbatia watendaji hali ambayo imesababisha kutokuwa na imani naye
Habari kwa hisani ya Rashid Mkwinda
|
1 comment:
Mtafukuza wangapi? je,nyie madiwani kazi
mnaweza? mbona katani kwenu matatizo-
tupu? mi nadhani madiwani hawa wametu
mwa ,fukuzeni hata walimu walevi basi!
Post a Comment