Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania Ilse Boshof akiwa ameshika mfuko wa saruji aina ya TemboFundi akiwa pamoja na Mkurugenzi wa masoko na mawasiliano |
Maafisa wa Lafarge wakionesha mifuko itakayotumika kuhifadhia Saruji ya TemboFundi |
Mkurugenzi wa Masoko na mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuzindua aina mpya ya saruji ya TemboFundi |
Meneja Mawasiliano wa Lafarge, Straton Bahati akizungumza namna watakavyoweza kuwafikia wateja na kutoa elimu kuhusu matumizi ya Saruji mpya ya TemboFundi |
Baadhi ya Watumishi wa Mbeya Cement wakishuhudia uzinduzi wa saruji aina ya TemboFundi |
Kikundi cha Burudani kikionesha mbwembwe zake katika uzinduzi wa Saruji ya TemboFundi |
KAMPUNI ya Saruji ya Mbeya
Cement(LAFARGE) imezindua aina mpya ya saruji ambayo haijawahi kupatikana
nchini Tanzania inayojulikana kwa jina la TemboFundi
kwa ajili ya shughuli za ujenzi.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzji wa Saruji ya TemboFundi, Mtendaji Mkuu wa Lafarge, Ilse Boshof,
alisema lengo la kuanzisha aina mpya ya saruji kumetokana na ushindani uliopo
sasa wa saruji hivyo kumetoa fursa kwao kubuni vitu vipya kwa manufaa ya jamii.
Alisema Saruji ya TemboFundi ni
maalum kwa kazi za kupigia plasata, kusakafia sakafu,kubandikia malumalu na
kuunganishia matofari wakati wa ujenzi jambo ambalo litamrahisishia mwananchi
kuepuka kutumia saruji tofauti na mahitaji.
Boshof alisema wazo la
kuleta aina hiyo mpya ya saruji
limetokana na maoni ya wateja ambapo wataalamu walifanya utafiti kwa muda
usiopungua miaka miwili hatimaye kufanikiwa kuanza kuzalisha aina hiyo.
Kwa upande wakeMkurugenzi wa
Masoko na Mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo, alisema changamoto kubwa ya
ushindani wa soko ndiyo iliyopelekea Lafarge kuendelea kuwa wabunifu kwa
kutafuta kile ambacho kinahitajika na wananchi.
Alisema zipo aina tofauti
tofauti za saruji zinazozalishwa katika kiwanda cha Mbeya ambazo kazi zake ni
tofauti pamoja na gharama ambapo saruji za wakandarasi wakubwa zinatofautiana
na saruji ya kutengenezea tofali za kujengea ambazo gharama zake ni kubwa
lakini uwepo wa TemboFundi itamrahisishia Mteja.
Naye Mkuu wa Ufundi, Mhandisi
Emily Sindatu alisema hivi sasa timu ya watumishi imejipanga kuwafikia wateja
wao kutoa elimu juu ya matumizi ya saruji kuanzia mafundi hadi wanunuaji ili
kupata ubora wa kitu anachokifanya.
Alisema nyumba nyingi hujengwa
chini ya kiwango na baadaye kubomoka hutokana na mafundi wengi kutokujua namna
ya kuchagua aina ya mchanga unaofaa kujengea pamoja na uchanganyaji kati ya
saruji na mchanga.
Aidha Meneja mawasiliano wa
Lafarge Mbeya alisema watatumia gari maalum kuitangaza aina mpya ya saruji kwa
kuzunguka barabarani, mitaani na kwenye mikusanyiko ya watu pamoja na
kuwatembelea mafundi kwenye maeneo yao na madukani zinapouzwa saruji ili kutoa
elimu.
No comments:
Post a Comment