Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, May 21, 2016

WAZEE WA CCM MBEYA WARIDHISHWA NA KASI YA RAIS MAGUFULI.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa CCM Jiji la Mbeya Isakwisa Mwambulukutu akisoma tamko la kumuunga mkono Rais Magufuli kwa utendaji wake.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa CCM Jiji la Mbeya Isakwisa Mwambulukutu akisoma tamko la kumuunga mkono Rais Magufuli kwa utendaji wake kwa wandishi wa habari.


Mmoja wa Wazee wa CCM Jiji la Mbeya akifuatilia kwa makini tamko la kumpongeza Rais Magufuli
Baadhi ya Wazee wa CCM wakifuatilia tamko lililosomwa na mwenyekiti wao la kumpongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake.

WAZEE wastaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jiji la Mbeya wamempongeza Rais wa awamu ya Tano Dk.John Magufuli katika juhudi zake za utekelezaji  mzuri wa ilani ya  uchaguzi mkuu wa 2015 na kuahidi kumuunga mkono.

Akisoma tamko mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa CCM Jiji la Mbeya, Isakwisa Mwambulukutu, alisema lengo la wazee kumpungeza ni juhudi zake ambazo ni kuboresha maisha ya kila mtanzania kwa kuhimiza ufanyaji kazi kwa bidii kwa kauli yake ya “hapa kazi tu”.

Alisema Rais Magufuli katika uongozi wake amesimamia uwajibikaji na uimarishwaji wa watumishi wa umma ambapo matokeo ya hivi sasa yameonesha mabadiliko kutoka kufanya kazi kwa mazoea katika sekta za umma hadi kuwa kwenye mfumo ambao kila mtu anaona serikali inawajibika.

Alisema maeneo mengine aliyosimamia Dk. Magufuli ni pamoja na kupambana na rushwa, ukwepaji kodi na ubadhilifu wa mali za umma kwa kutumbua majipu, kuboresha huduma za jamii ili kuleta hali nafuu ya maisha ya watanzania kama huduma za Hospitali na elimu bure kuanzia awali hadi sekondari .

Aliongeza kuwa suala la kufufua na kuhimiza ujenzi wa viwanda jambo ambalo litachangia ongezeko la vijana kupata ajira hivyo kupunguza uwezekano wa kukaa bila kufanya kazi na kujiingiza kwenye vitendo viovu.

“Katika sekta ya viwanda ni vema akatupia jicho katika viwanda ambavyo vimekufa jijini Mbeya kama vile kilichokuwa cha kutengeneza sabuni (HISOAP), kutengeneza zana za kilimo(ZZK), kiwanda cha nguo(Mbeya textile) na kiwanda cha Nyama cha Tanganyika Peakers.

Wazee hao mbali na kumpongeza Rais katika maeneo hayo pia walimuomba Dk. Magufuli kuhakikisha anasimamia vema suala la matibabu bure kwa wazee kwani mbali na uwepo wa utaratibu huo lakini huduma wapatayo hairidhishi.

Walisema ili waweze  kumudu matibabu kiurahisi ni vema Serikali ikawaingiza kwenye mfumo wa Mfuko wa bima ya afya ya Tifa ili kuwarahisishia kuweza kupata matibabu katika Hospitali zozote bila kutegemea sehemu moja ya Hospitali ya Serikali.

Waliongeza kuwa wanaomba pia Wazee wote ambao hawalipwi pensheni kwa vile hawakuwa watumishi wa umma walipwe ili kuwapunguzia makali ya maisha pia kuwaboreshea wale ambao wako kwenye mfumo kulingana na wakati.


No comments: