Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, May 20, 2016

MISS MBEYA 2016 KUJULIKANA LEO MEI 20 PARADISE HOTEL

Washiriki wa shindano la walimbwende la Miss Mbeya City 2016 wakiwa katika pozi wakati wa kikao cha mratibu wa mashindano hayo yatakayofanyika  Ijumaa(Mei 20) Tom Chilala na wanahabari.

Mratibu wa mashindano ya Miss Mbeya 2016 Tom Chilala akifafanua jambo kwa wanahabari waliohudhuria kikao cha maandalizi kilichofanyika katika Hoteli yaBeaco jijini MbeyaWashiriki wa shindano la walimbwende la Miss Mbeya City 2016 wakiwa katika pozi wakati wa kikao cha mratibu wa mashindano hayo yatakayofanyika kesho Ijumaa(Mei 20) Tom Chilala na wanahabari.

MRATIBU wa Shindano la kumsaka mrimbwende wa kuuwakilisha Mkoa wa Mbeya katika kumsaka miss Tanzania  2016, Tom Chilala amejinasibu taji hilo kunyakuliwa na mrembo kutoka Mbeya.
 
Aidha shindano hilo linalotarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Paradise jijini Mbeya linatarajia kuwashirikisha Warembo  11 kati ya 15 waliojitokeza kuwania  taji la Miss Mbeya 2016 watapanda  jukwaani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Tom Chilala alisema anajivunia rekodi ya kuandaa mashindano hayo mahali tofauti na washindi wake huchukua taji hilo la Tanzania.
 
Alisema awali waliojitokeza katika kinyang`anyiro hicho walikuwa warembo 15  kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya lakini ulifanyika mchujo wa awali  na kubakia warembo 11 ambao ndiyo watapanda jukwaani.
 
Alisema mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia fedha tasilimu Sh 700,000,wa pili Sh400,000,wa tatu Sh300,000 na mshindi   wa nne Sh200,000 huku wa tano hadi wa 11 watapata kifuta jasho Sh 80,000.
 
Alisema shindano hilo mwanamuziki   chipukizi anayetamba kwa sasa katika muziki wa Bongo  Fleva Rajabu Abdulkhali (Harmonizer) anatarajia kutumbuiza na kwamba mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
 
Chilala amewataja warembo watakaopanda jukwaani ni pamoja na Emiliana Abdalah,Anitha Parick,Aziza Lyasamuya na Praxeda Geofrey.
 
Wengine ni Juliana Gilbert,Nancy Matta,Agnes Boliva,Julitha Mponela,Afrodisia Chapa,Eunice Robert,Pricar Mengi na Juliana Lyampawe.
 
Kwa upande wao baadhi ya warembo watakaoshindana walijinasibu kuwa mmoja wao atakayepita kutoka Mbeya ndiye atakayenyakua taji hilo kutokana na sifa walizonazo.
 

No comments: