Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, May 20, 2016

MBEYA CEMENT (LAFARGE) YAZINDUA AINA MPYA YA SARUJI RAFIKI KWA MAFUNDI

 
Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania Ilse Boshof akiwa ameshika mfuko wa saruji aina ya TemboFundi akiwa pamoja na Mkurugenzi wa masoko na mawasiliano

Maafisa wa Lafarge wakionesha mifuko itakayotumika kuhifadhia Saruji ya TemboFundi

Mkurugenzi wa Masoko na mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuzindua aina mpya ya saruji ya TemboFundi

Meneja Mawasiliano wa Lafarge, Straton Bahati akizungumza namna watakavyoweza kuwafikia wateja na kutoa elimu kuhusu matumizi ya Saruji mpya ya TemboFundi

Baadhi ya Watumishi wa Mbeya Cement wakishuhudia uzinduzi wa saruji aina ya TemboFundi




Kikundi cha Burudani kikionesha mbwembwe zake katika uzinduzi wa Saruji ya TemboFundi

KAMPUNI ya Saruji ya Mbeya Cement(LAFARGE) imezindua aina mpya ya saruji ambayo haijawahi kupatikana nchini Tanzania inayojulikana kwa jina la TemboFundi kwa ajili ya shughuli za ujenzi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzji wa Saruji ya TemboFundi, Mtendaji Mkuu wa Lafarge, Ilse Boshof, alisema lengo la kuanzisha aina mpya ya saruji kumetokana na ushindani uliopo sasa wa saruji hivyo kumetoa fursa kwao kubuni vitu vipya kwa manufaa ya jamii.

Alisema Saruji ya TemboFundi ni maalum kwa kazi za kupigia plasata, kusakafia sakafu,kubandikia malumalu na kuunganishia matofari wakati wa ujenzi jambo ambalo litamrahisishia mwananchi kuepuka kutumia saruji tofauti na mahitaji.

Boshof alisema wazo la kuleta  aina hiyo mpya ya saruji limetokana na maoni ya wateja ambapo wataalamu walifanya utafiti kwa muda usiopungua miaka miwili hatimaye kufanikiwa kuanza kuzalisha aina hiyo.

Kwa upande wakeMkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo, alisema changamoto kubwa ya ushindani wa soko ndiyo iliyopelekea Lafarge kuendelea kuwa wabunifu kwa kutafuta kile ambacho kinahitajika na wananchi.

Alisema zipo aina tofauti tofauti za saruji zinazozalishwa katika kiwanda cha Mbeya ambazo kazi zake ni tofauti pamoja na gharama ambapo saruji za wakandarasi wakubwa zinatofautiana na saruji ya kutengenezea tofali za kujengea ambazo gharama zake ni kubwa lakini uwepo wa TemboFundi itamrahisishia Mteja.

Naye Mkuu wa Ufundi, Mhandisi Emily Sindatu alisema hivi sasa timu ya watumishi imejipanga kuwafikia wateja wao kutoa elimu juu ya matumizi ya saruji kuanzia mafundi hadi wanunuaji ili kupata ubora wa kitu anachokifanya.

Alisema nyumba nyingi hujengwa chini ya kiwango na baadaye kubomoka hutokana na mafundi wengi kutokujua namna ya kuchagua aina ya mchanga unaofaa kujengea pamoja na uchanganyaji kati ya saruji na mchanga.

Aidha Meneja mawasiliano wa Lafarge Mbeya alisema watatumia gari maalum kuitangaza aina mpya ya saruji kwa kuzunguka barabarani, mitaani na kwenye mikusanyiko ya watu pamoja na kuwatembelea mafundi kwenye maeneo yao na madukani zinapouzwa saruji ili kutoa elimu.


No comments: