Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 22, 2016

BENKI YA NMB YAZINDUA KITUO CHA BIASHARA MBEYA

Mwonekano wa Jengo la Nmb Business Center lililopo Mwanjelwa Mbeya
Meneja wa Nmb Business Center Mbeya Bi Mary Ngalawa akimwonesha Mkurugenzi mkuu wa Nmb Tanzania Nzima Bi Ineke Bussemaker sehemu Mbalimbali za Jengo hilo..


Mkuu wa idara ya Biashara Bw James Meitaros akielezea jambo kwa Mkurugenzi mkuu wa Nmb Tanzania Nzima Bi Ineke Bussemaker.

Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kwa wateja Bw Abdul Majid Nsekela akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi mkuu wa Nmb Tanzania Nzima Bi Ineke Bussemaker..
Wafanyabiashara wa Jiji la Mbeya .
Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kwa wateja Bw Abdul Majid Nsekela akizungumza na Wafanyabiashara.

Mkurugenzi mkuu wa Nmb Tanzania Nzima Bi Ineke Bussemaker akiwakaribisha wafanyabiashara walifika katika Ufunguzi huo wa Nmb Business Center Mbeya


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Abbas Kandoro ndiyo Ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Nmb Business Center Mbeya..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi na wafanyabiashara..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi na wafanyakazi wa Nmb..(Picha kwa hisani ya Fahari News Blog)Benki ya NMB imezindua kituo cha biashara (NMB BUSSINESS CENTER) katika mkoa wa Mbeya kitakachokuwa kikiinua na kuboresha uendeshaji wa biashara kwa wafanya biashara katika mkoa huo.
Akiongea kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi wa wateja wa NMB Tanzania Abdulmajid Nsekela amesema kuwa lengo la vituo vya biashara kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini ni kufanikisha kufanya shughuli zao na kupata elimu bora ya kifedha na wanataraji kuendelea kuwafikia wafanyabiashara popote walipo kwa huduma bora.
Aidha mkurugenzi huyo wa wateja ameeleza kuwa katika mpango huo wanataraji kufanikisha malengo ya wateja wao ambao ni wafanyabiasha wakubwa , wakati , wadogo sambamba na wakulima kwa kuboresha biashara ya kilimo.
Pia Nsekela amefahamisha kuwa pamoja na kufanya shughuli za kibenki pia wanachangia shughuli za kijamii katika kuchangia maendeleo na wanatenga pato lao la mwaka kwa kuchangia sekta ya afya na elimu ikiwa na lengo la kuiunga mkono serikali ambapo wanatenga asilimia moja katika pato la mwaka kufanya shughuli hizo.
Mkurugenzi huyo wa wateja kwenye benki ya NMB Tanzania amewataka wateja wa kati kuchangamkia fursa hiyo ambayo inawapa nafasi wafanya biashara kupanda kutoka daraja moja kwenda lingine kulingana na ufanisi wa vituo vya biashara na elimu ya kifedha watakayopatiwa na NMB.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha biashara cha NMB mkoa wa Mbeya ambaye   pia ni mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka wafanyabiasha na wakazi wa mkoa huo kuitumia fursa za kibenki ambazo zinatolewa ili kufikia malengo yao ya kibiashara.
Kandoro amefahamisha kuwa kabla ya kuchukua mkopo wanatakiwa kufanya tathimini na kujua biashara gani ambayo wanaweza kufanya na kuweza kurejesha marejesho ya benki.
Pia Kandoro aliwataka viongozi wa benki ya NMB kuangalia suala la riba katika mikopo wanayotoa kwa vile wananchi wengi wanaogopa kukopa kutokana na baadhi ya mabenki nchini kutoza riba kubwa jambo linalowawia vigumu wafanyabiasha wadogo kujenga kasumba ya kuhofia mikopo kwa ajili yakujiendeleza kichumi na kupanua wigo wa biashara zao.
Benki ya NMB pia imejikita kwenye shughuli za kilimo kwa kuwezesha urahisi wa upatikanaji wa pembejeo ambapo hivi karibuni wameanzisha mpango wa kuwapatia wateja wake matrekta kwa bei rahisi baada ya kuingia mkataba na kampuni ya Jebiz ambao ni wasambazaji wa matrekta
Pia NMB inamatawi 175 ATM zaidi ya 600 mawakala ambao wanarahisisha shughuli za kibenki zaidi ya 450 na wamejiunga na mitandao ya kifedha ya makampuni ya simu yote
Kwa upande wa mikopo mkuu wa kitengo cha biashara James Meitaron ameeleza utaratibu mzima wa utoaji wa mikopo kiwango ambacho wanaanzia kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuanzia shilingi milioni moja mpaka milioni thelathini(milioni 30) mkopo ambao unapatikana ndani ya siku mbili ambapo benki hiyo imempa mamlaka meneja wa tawi kufanikisha mikopo ya kiwango hicho.
kama biashara yako imeanza kukua kituo cha biashara ambapo kwa mbeya kipo NMB Mwanjelwa wanatoa mkopo kuanzia milioni 30 mpaka bilioni 2.
Amesema  Meitaron  kuwa riba ya mikopo kwa benk hiyo haizidi asilimia 23 kwa mwaka na kadri unavyolipa mkopo riba inapungua mpaka kufikia asilimia 18 kulingana na mkopo uliokopa.

No comments: