Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, January 22, 2016

TAJATI YAFANYA ZIARA WILAYA YA CHUNYA NA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII

Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Chunya, Dk. Ano Maseta akitoa taarifa fupi kuhusiana na hali ya Hospitali hiyo baada ya kupokea ugeni wa Waandishi kutoka Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI).

Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili akitoa taarifa juu ya Safari ya Wanachama wa TAJATI Wilaya ya Chunya kwa Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya(hayupo pichani)


WanaTAJATI walipata fursa ya kutembelea wagonjwa na kutoa msaada kidogo katika Wodi la Wazazi na Watoto, Pichani ni Ezekiel Kamanga mwanachama wa TAJATI akimpa pole mgonjwa katika wodi la wazazi
WanaTAJATI pia walipata fursa ya kushiriki upandaji wa miti kuzunguka eneo la Hospitali ambapo miti zaidi ya 50 ilipandwa


Mbali na kupanda miti pia walifanya usafi katika mazingira yanayoizunguka Hospitali ya Wilaya ya Chunya

TAJATI wakishiriki ujenzi wa daraja kubwa lililojengwa kwa nguvu za wananchi wa Kijiji cha Igangwe kata ya Mtanila Wilaya ya Chunya linaloviunganisha vitongoji vya Shauri Moyo na Mtukula

Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili akishirikiana na Mwenyekiti wa Igangwe Amcos kuzindua zoezi la upandaji wa miti katika Shamba la Chama cha Msingi cha Igangwe ambapo miti zaidi ya 1000 ilipandwa

Wakulima wa Igangwe amcos wakishirikiana na Wanachama wa TAJATI katika upandaji wa miti

Makamu Mwenyekiti wa TAJATI, Christopher Nyenyembe akikagua timu za mpira wa miguu kabla ya kuanza kwa mtanange katika kuadhimisha mapinduzi ya Zanzibar


Mtunza Hazina wa TAJATI, Brandy Nelson akimkabidhi zawadi nahodha wa timu ya msindi wa Kwanza katika mechi maalum ya kuenzi mapinduzi ya Zanzibar

Katibu Mkuu wa TAJATI, Venance Matinya, akimkabidhi zawadi ya mpira wa miguu nahodha kwa niaba ya timu yake baada ya kuibuka kidedea katika shindano maalum la kuenzi mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika Lupa wilayani Chunya

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli akiwa katika kikao cha majumuisho ya ziara ya waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI).

Makamu Mwenyekiti wa TAJATI akiagana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
 
 
BAADHI ya Wanachama wa Chama  cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) walifanya ziara ya siku tatu katika Wilaya ya Chunya na kushiriki shughuli mbali mbali za kijamii na kihabari.
 
Waandishi hao walifanya ziara hiyo jumatatu na kukamilisha jumatano ya wiki hili ambapo wakiwa Wilayani Chunya walipokea taarifa ya hali ya utalii ya Wilaya ya Chunya na kushiki shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
 
Akizungumza katika majumuisho ya Ziara hiyo iliyojumuisha waandishi 12, mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli, Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili alisema katika ziara hiyo iliyokuwa na mafanikio imepokelewa vizuri na wananchi.
 
Alisema siku ya kwanza waandishi waliweza kutembelea wagonjwa na kutoa zawadi kidogo ikiwemo sabuni za kufulia na vinywaji aina ya Grandmalt kwa ajili ya kuongeza nguvu sambamba na usafi wa mazingira ulioenda sambamba na uzinduzi wa kupanda miti ambapo miti zaidi ya 50 ilipandwa kati ya 560 inayotarajiwa kupandwa na Hospitali hiyo.
 
Aliongeza kuwa siku ya pili waandishi hao walishiriki katika ujenzi wa daraja la Mto Lupa katika Mto kijiji cha Igangwe linalounganisha Kijiji hicho na Vitongoji wa Shauri Moyo na Mtukula lenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Mbili.
 
Aliongeza kuwa baada ya kushiriki ujenzi wa daraja hilo waandishi hao pia walijumuika na wakulima wa Chama cha Msingi cha Igangwe Amcos katika zoezi la upandaji wa miti ambapo zaidi ya miti laki moja ilipandwa ikiwa ni kutekeleza utunzaji wa mazingira na kampeni ya kata mti  panda miti.
 
Zoezi hilo la upandaji miti limetokana na wakulima wa Tumbaku kutumia miti kwa kiasi kikubwa wakati wa kuandaa zao la Tumbaku hadi mavuno jambo lililopelekea uongozi wa Amcos kuweka sheria na kanuni kwa kila mkulima kuhakikisha anapanda miti 500 katika shamba la Chama cha msingi na 25 shambani kwake.
 
Mwakilili alisema mbali na kushiriki shughuli hizo pia waandishi walizungumza na wananchi kuhusu changamoto zinazowakabili ambapo mambo mengi yalibainishwa ikiwemo ndoa za utotoni, mimba mashuleni na upungufu wa wahudumu wa afya katika kituo cha Afya Mtanila ambacho kina watumishi wanne tu.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Sophia Kumbuli mbali na kuwapongeza WanaTAJATI  kwa ziara yao pamoja na shughuli zingine za kimaendeleo na kijamii aliahidi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyobainishwa.
 
Kuhusu ndoa za utotoni Mkurugenzi alisema atawasiliana na Kamati ya Ulinzi na uasalama ya Wilaya ili kuanza utekelezaji wa kuwasaka wanaume wanaooa mabinti wadogo na kuwakatika katika masomo yao.
 
Alisema suala la afya kutokuwa na watumishi wa kutosha alisemahilo ni tatizo la Wilaya nzima ingawa Serikali inatarajia kutangaza nafasi za kuajiri hivyo tatizo hilo linaweza kupungua kwa kiasi Fulani.
 
“Niwapongeze kwa juhudi zenu na ninawaahidi kuyafanyia kazi mambo yote mliyoyabaini mkiwa Wilayani Chunya hususani suala la kuozesha watoto wadogo hili limenisikitisha mno na sitalifumbia macho nitatoa taarifa kwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ili wahusika wasakwe mara moja huu ni ukatili wa kijinsia” alisisitiza Mkurugenzi.
 

No comments: