Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 1, 2016

KANDORO AZINDUA WIKI LA SHERIA NCHINI MKOA WA MBEYA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na wananchi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini

Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya, Jaji Noel Chocha akielezea malengo ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho hayo


Baadhi ya Wanasheria na Mahakimu wa Mahakama za Mkoani Mbeya wakiwa katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria nchini iliyozinduliwa kimkoa katika Stendi ya daladala Kabwe jijini Mbeya


Baadhi ya wananchi wakifuatilia uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria nchini yaliyofanyika katika kituo cha daladala jijini Mbeya

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro  amezindua rasmi wiki ya sheria nchini inayoadhimishwa kimkoa katika kituo cha daladala Kabwe jijini Mbeya.

Katika uzinduzi huo Kandoro ametoa wito kwa wananchi kuwaepuka watu wanaojiita wanasheria wa mitaani(power of attoney) kwani wanachelewesha na kupotosha upatikanaji wa haki kutokana na kufanya kazi kwa njia ya utapeli.

Kandoro alisema wananchi kupitia wiki hili wajitahidi kuhudhuria kupata mafunzo juu ya njia mbali mbali za kupata haki badala ya kuwatumia matapeli wa mitaani wanaowadanganya na kuwatapeli.

“Hawa wanaojiita power of attoney tunapaswa kuwaepuka sana pia tulitumie wiki hii kujifunza njia sahihi za kufuata kupata haki kwani hawa watu ni matapeli ndiyo wanatengeneza mianya ya rushwa na kula fedha za mlala hoi kwa kutokujua haki na njia sahihi” alisema Kandoro.

Aidha alitoa wito kwa Mawakili wa kujitegemea kupunguza gharama za kuendeshea kesi ili kuwawezesha wananchi wenyekipato cha chini kuweza kumudu kupata msaada wa kisheria kutoka kwa mawakili.

Alisema kutokana na gharama za mawakili kuwa kubwa ndiyo inayosababisha vishoka wa sheria kuibuka mitaani kwa ajili ya kumpunguzia gharama mlalamikaji ili aweze kupata msaada kwa gharama ndogo.

Alisema pia wanapaswa kufungua matawi vijijini na sio kubaki mjini ili kuweza kufikia maeneo mengi kwa wakati sahihi sambamba na kuwafikia wananchi wengi.

Awali akimkaribisha mkuu wa Mkoa, Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Jaji Noel Chocha alisema katika siku tatu za maadhimisho ya wiki ya sheria itakayohitimishwa Februari 4, mwaka huu itaenda sambamba na utoaji wa elimu juu ya maswala ya sheria kwa wananchi.

Jaji Chocha alisema maadhimisho hayo hayajawahi kufanyika kwa kutoa elimu kwa wananchi hivyo itakuwa endelevu kila mwaka ambapo katika maadhimisho hayo elimu itatolewa na mawakili wa Serikali, mawakili wa kujitegemea, Jeshi la Polisi, idara ya ardhi na migogoro na ustawi wa jamii na dawati la jinsia.

Alisema maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya Wajibu wa Mahakama na wadau katika utoaji wa haki  itafanyika katika vituo viwili katika Jiji la Mbeya ambavyo ni vituo vya mabasi vya Kabwe na Nanenane.

No comments: