Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, January 19, 2016

AIRTEL MKWANJIKA YATUA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, WASHINDI NANE WAJIZOLEA FEDHA.

Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akipewa maelezo kabla ya kuingia kwenye boksi la kuokota fedha katika shindano la kwangua ushinde


Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akiwa kwenye boksi la kuokota fedha katika shindano la kwangua ushinde akiendelea kujikusanyia mapesa.

Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akishuhudia fedha alizookota zikihesabiwa katika shindano la kwangua ushinde

Iddi Yusufu akiendelea kuokota fedha katika boksi kwenye shindano la kwangua ushinde na Airtel Mkwanjika

Mshindi  Jotham Mwainyekule akijaribu bahati yake kama anaweza kuokota fedha zote ambazo ni shilingi Milioni Moja anazopaswa kuziokota kwa muda wa sekunde 60

Menena Mauzo wa Airtel Kanda ya Nyanda za juu kusini, Straton Mushi akielezea namna zoezi la Kwangue ushinde linavyofanyika na washindi wanavyopatikana ambapo kwa Kanda jumla ya washindi nane wamepatikana



Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakishuhudia shindano la Kwangua ushinde la Airtel Mkwanjika

Mshereshaji wa Airtel Mkwanjika akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa shindano kwa washindi kuokota fedha

Mmoja wa Watumishi wa Airtel akionesha mfano jinsi ya kushiriki zoezi la kuokota fedha linavyopaswa kufanyika


PROMOSHENI inayoendeshwa na Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel inayojulikana kwa jina la Kwangua ushinde na Airtel Mkwanjika imetua katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini ambapo washindi nane wamepatikana na kujizolea fedha taslimu.

Zoezi la kuwapatia zawadi washindi hao lilifanyika jana katika ofisi za Kanda za Airtel zilizopo Uhindini Jijini Mbeya na kushuhudiwa na wakazi wa Jiji hilo kutokana na zoezi hilo kufanyika katika maeneo ya wazi.

Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Nyanda za juu kusini, Straton Mushi alisema tangu shindano hilo lianze mwezi Disemba mwaka jana nchi nzima wateja wengi wamejitokeza na kujizolea fedha lukuki ambazo zimekuwa zikiwasaidia katika kuboresha hali yao ya kiuchumi kwa kuongeza vipato vyao.

Alisema hakuna masharti yoyote ya mteja kujishindia bali anachopaswa ni kununua vocha na kuikwangua kasha kuijaza kwenye simu yake ya Airtel anakuwa ameingia moja kwa moja kwenye shindano ambapo baada ya kuchaguliwa huingizwa kwenye boksi maalum lenye fedha taslimu shilingi Milioni moja ambazo hupulizwa na upepo hivyo kasi ya mteja kuokota fedha ndizo zinakuwa zawadi yake.

Aliwataja washindi walioshiriki kujiokoteza fedha kwa Kanda kuwa ni pamoja na Ismail Mwaswale (Sumbawanga) ambaye kwenye boksi alijiokotea jumla ya shilingi 920,000 kwa muda wa sekunde sitini akifuatiwa na Iddi Yusufu (Iringa) aliyeokota shilingi 750,000 na Jotham Mwainyekule mkazi wa Mbozi aliyepata shilingi 730,000/=.

Aliwataja washindi wengine kuwa ni Kazembe Salamanda Mkazi wa Ruvuma, Onesmo Lubaga mkazi wa Iringa, Tonny Moris Mkazi wa Mbeya, Bahati Muhawala mkazi wa Mbeya na Thomas Baraka mkazi wa Rukwa ambao viwango vyao havikujulikana mara moja.

Wakizungumza baada ya kumalisha shindano hilo washindi hao walitoa wito kwa watanzania kuiamini Airtel na kuitumia kwa kuwa huduma zao ni za kweli na uhakika tofauti na madai ya wengi kuwa promosheni hizo ni danganya toto.

Ismaila Mwaswale(43)Mkazi wa Sumbawanga na mfanyabiashara mdogo alisema baada ya kupigiwa simu kwamba ameshinda hakuamini hadi pale alipotumiwa nauli ya kuja kushiriki zoezi hilo mkoani Mbeya.

Alisema fedha alizopata zitamsaidia kuongeza mtaji wa biashara yake ambayo imekuwa ikisuasua kutokana na mtaji mdogo huku fedha zingine akizielekeza kulipia karo za watoto wanaosoma shule binafsi.

Iddi Yusuph (26) mkazi wa Iringa alisema ni vema Watanzania na wateja wa Airtel wakaamini kuwa kichezo hiyo ipo na inafanyika kweli wala sio utapeli na haifanyiki kwa kujuana na watumishi wa airtel kwani yeye mwenyewe ameshinda pasipo kutoa chochote wala kujuana na mtumishi yeyote.

Baadhi ya mashuhuda wa mashindano hayo walisema ni jambo zuri linalofanywa na Kampuni ya Airtel kwa kuweka mashindano ya wazi ambapo kila mtu anaona namna mshiriki anavyohangaika kuokjota fedha kutoka kwenye boksi na kwamba hali hilyo huonesha kuwa hakuna upendeleo.



No comments: