Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, January 2, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII AOMBA USHIRIKIANO KUIBORESHA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA.


Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Afya Dk. Mpoki Ulisubisya (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Donan Mbando(katikti) wakijadili jambo katika moja ya ziara ya kushtukiza aliyoifanya mwezi Disemba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wakati huo Dk. Ulisubisya akiwa Mkurugenzi wa HospitaliKATIBU mkuu wa Wizara ya Afya na ustawi wa jamii ambaye awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini, Dk. Mpoki Ulisubisya amesema ushirikiano unatakiwa ili kutekeleza mambo mbali mbali aliyoyaacha.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya, Dk. Ulisubisya alisema hakutarajia kama Rais Dk. Magufuli angeweza kumpa majukumu na kumteua katika nafasi kubwa jambo lililomshtua kwa kiasi kikubwa.

Alisema kichwani kwake alikuwa anajipanga kuhakikisha anatekeleza majukumu aliyokuwa ameachiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya afya na ustawi wa jamii wiki mbili zilizopita Donan Mbando aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda.

Alisema katika ziara hiyo Mbando aliagiza kuhakikisha umaliaziaji wa jingo la maabara ya kupima virusi vya Ebola unakamilika haraka ndani ya wiki mbili na kuanza kutoa huduma, ujenzi wa jengo la vipimo mbali mbali kama Utra  saund, CT Scan na X – Ray.

Alisema agizo lingine lilikuwa kuhakikisha Hospitali hiyo inaanzisha Chuo kikuu kwa ajili ya kuongezea taaluma kwa madaktari na kuboresha huduma za dharura na kupunguza foleni kwa wagonjwa mambo ambayo tayari alianza kuyafanyia kazi na kuyawekea mikakati.

Aidha alitoa wito kwa waandishi wa habari kuendelea kuandika habari za kuisaidia hospitali na madaktari ili waweze kurekebisha kasoro zinazokuwepo lengo likiwa ni kuhakikisha Hospitali hiyo inakuwa mfano kitaifa kwa utoaji wa huduma bora.

Dk. Ulisubisya  pia alitoa wito kwa waandishi wa habari kuendelea kumpa ushirikiano Mkurugenzi mwingine atakayechukua nafasi yake ili kuhakikisha mipango yote inakamilika kama ilivyokuwa imepangwa.

No comments: