Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, January 4, 2016

KIJANA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA KANDO KANDO YA MTAA WA MWAMFUPE, JIJINI MBEYA


Baadhi ya Wanachi wa Mtaa wa Mwamfupe wakijadiliana jambo katika Eneo la Tukio.
Huzuni  umetawala Eneo hilo..
Wanachi sambamba na Wenyenyumba zilizo zunguka Eneo hilo la Tukio wakisubiri msaada kutoka Jeshi la Polisi.
Picha na Fadhiri Atick - Mr.Pengo Mbeya.

Kijana Mmoja ambaye hajaweza fahamika Majina yake, amekutwa akiwa amefariki Dunia kwenye kichochoro maeneo ya Mtaa wa Mwamfupe, Jijini Mbeya leo asubuhi. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walieleza kuwa Mapema leo Asubuhi waliukuta Mwili huo katika Eneo hilo, na kueleza kuwa "Mtu huyo si Mkazi wa Eneo hilo bali Jioni ya jana waliomuona Mazingira hayo akiwa katika hali ya kupepesuka Pepesuka kotokana na unywaji wa Pombe kwa kiwango kilichopitiliza na huenda hicho ndicho kilicho pelekea Kifo chake kwani alikuwa si Ngangali katika Afya..." hivyo ndivyo walivyo sema wana  Mtaa wa Mwamfupe walipo kuwa wakizungumza na Mwandishi wetu.

CHANZO MICHUZI MEDIA GROUP

No comments: