Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, December 28, 2015

SHIVIWAKA WAITAKA SERIKALI KUPUNGUZA MLUNDIKANO WA KODI KWENYE KAHAWA

Kaimu Mkurugenzi wa SHIVIWAKA, Ezekia Mwakasungula akitoa mada wakati wa mafunzo ya  kuwajengea uwezo na kubadilishana uzoefu  katika masuala ya utawala bora na uwajibikaji baina ya uongozi wa shirikisho hilo na waandishi wa habari mkoani Mbeya.


Mwenyekiti wa SHIVIWAKA, Edward Masawe akifungua  mafunzo ya  kuwajengea uwezo na kubadilishana uzoefu  katika masuala ya utwala bora na uwajibikaji baina ya uongozi wa shirikisho hilo na waandishi wa habari mkoani Mbeya.

Baadhi ya viongozi wa Shiviwaka wakiwa kwenye mafunzo

Baadhi ya Wandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mafunzo

Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye picha ya pamoja.


SHIRIKISHO la Vikundi vya wakulima wa Kahawa Tanzania lenye makao makuu Mkoa wa Mbeya  (SHIVIWAKA) limeiomba Serikali kuondoa mlundikano wa kodi katika zao la kahawa.
 Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni na  Mwenyekiti wa SHIVIWAKA, Edward Masawe wakati wa mafunzo ya  kuwajengea uwezo na kubadilishana uzoefu  katika masuala ya utwala bora na uwajibikaji baina ya uongozi wa shirikisho hilo na waandishi wa habari mkoani Mbeya.

Massawe alisema hivi sasa kuna zaidi ya kodi tatu ambazo mkulima hulipa moja kwa moja tangu kuanza kuotesha miche hadi mavuno jambo ambalo halisaidii kuinua uchumi wa Mkulima wa Kahawa nchini.

Alizitaja kodi hizo kuwa ni mchngo wa utafiti ambao mkulima hukatwa asilimia 0.75 ya dola   kwa kilo moja kwa mwaka wakati wa mavuno kulingana na soko lililopo mnadani.


Alisema tozo nyingine ni changizo la ushuru wa kila Halmashauri zinazolima zao la Kahawa ambapo mkulima huchangia asilimia 5 ya bei iliyopo mnadani.


Mwenyekiti huyo alisema kodi ya tatu ni changizo la maendeleo ya kahawa  ambayo ilibuniwa na kusimamiwa na bodiya kahawa kwa ajili ya pembejeo lakini badala yake fedha hizo huishia kwenye posho za vikao vya bodi.


Aliongeza kuwa malipo mengine ni gharama za magunia ya kusafirishia kahawa nje ya nchi ambayo ni dola 2.5 kwa kila gunia hivyo kumfanya mkulima kushindwa kuuza kahawa yake nje ya Nchi.



 Naye Makamu Mwenyekiti wa SHIVIWAKA, Rabon Mbegunyingine njema alisema wakulima wadogo wa zao la kahawa wamekuwa wakinyonywa kwa muda mrefu  kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu stahiki juu ya uhakika wa soko pamoja na bei elekezi hivyo umefika wakati sasa serikali ikaingilia kati suala hilo .


Mwenyekiti huyo amebainisha wazi kuwa endapo serikali itaamua kuingia kati na kuzungumza  moja kwa moja wakulima hao  kutasaidia kuibua na kufahamu changamoto wanazo kutana nazo  badala ya kuiachia jukumu hilo bodi ya kahawa ambao nao wamekuwa kikwazo kwa wakulima hao.


Aidha mmoja wa wajumbe  wa bodi hiyo ya SHIVIWAHAKA ambaye pia ni katibu wa Muungano group kutoka Utengule –Usongwe, Zakaria Mwashitete, alisema mkulima anapewa fedha kidogo tofauti na bei inayokuwepo sokoni.


Alisema changamoto hiyo inatokana na baadhi ya wajumbe wa bodi ya kahawa kumiliki makampuni ya kununulia kahawa hivyo kujipangia bei.

No comments: