Mkuu wa Wilaya ya Chunya Elias John Tarimo akizindua Mradi wa Kisima cha Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
Wananchi
wa kata ya Ngwala wilayani Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kutunza
miundo mbinu inayojengwa katika kata yao hasa miradi ya maji ili
waepukane na adha mbalimbali za kurudi katika adha walizokuwa wakipata
mwanzo.
Haya
yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Chunya Elias John Tarimo akiwa Mgeni
rasmi wakati akizindua visima viwili vilivyojengwa na kampuni ya peak
Resource limited ambayo hujihusisha na utafiti wa madini adimu chini ya
ardhi yanayopatikana katika kata ya ngwala wilayanii chunya mkoani
mbeya ambayo hutumika kutengenezea sumaku,mota,compyuta umeme wa
sumaku,simu ambayo kwa tanzania tanapatikana wilaya ya Chunya pekee.
Tarimo
alisema wananchi hawana budi kutunza miundo mbinu hiyo waliojengewa
kwani wakiiharibu watarudi katika adha ya shida ya maji walikuwanayo
hapo awali na kwamba waendeleze ushirikiano bora na kampuni hiyo kwani
mahusiona mema ndiyo chanzo cha mafanikio ya kupata maendeleo katika
kata yao.
Akisoma
tarifa fupi ya ujenzi wa miradi mbalimbali waliojenga katika kata hiyo
meneja mradi wa Peak Resource limited Patrick Ochieng alisema miradi
waliojenga ni visima viwili vilivyogharimu milioni 16kila kimoja unjezi
wa nyumba ya mwalimu iliyogharimu shilingi milioni 55 na ujenzi wa eneo
la kupumzikia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Ngwala iliyogharimu
shilingi milioni 7 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 94.
Ochieng
alindelea kueleza kuwa kwa sasa Kampuni yao ipo katika hatua za mwisho
za utafiti na kwamba wanafwatilia leseni ya uchimbaji madini na kibali
kutoka nemki ili kuanza uzalishaji na kwamba mgodi huo unauwezo wa
kudumu kuchimbwa kwa miaka 40.
Aidha
baadhi ya waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa miradi ni pamoja
na Mwenyekiti wa kijiji cha Neston Simoni na Diwani wa Kata ya Ngwala
Donard Maganga ambao walisema wamefurahishwa na kile kinachofanywa na
kampuni hiyo kwani wanajenga miradi bora kwa kutumia gharama nafuu.
Maganga
aliwataka wakazi wa Ngwala kuiga mfano wa kampuni hiyo kwani nalisema
nyumba waliojenga ya shilingi milioni 55 ukiweka Mkandarasi wangeweza
kujenga kwa shilingi milioni 100 hivyo alisema mfano wa kampuni hiyo
unapaswa kuigwa ili kuondoa ufisadi katika jamii yetu.
Kwaupande
wa wananchi waliokuwepo hapo walishukuru kampuni hiyo kwa kupunguza
adha walizokuwa nazo katika Kata yao kwani kwasasa wamekuwa na matumaini
wa kupata walimu ambao watafundisha watoto wao katika mazingira yalio
bora kutokana na uwepo wa nyumba bora ya Mwalimu ukilinganisha na hapo
awali walikuwa wanakosa eneo la kujihifadhi,alisema Raisoni George.
Vile
vile Elizabeti Yusuph mkazi wa ngwala alisema wao kama wakinamama
walikuwa wachelewa kufanya shughuli za shambani kutokana na kufwata maji
umbali mrefu kwani kutokana na uwepo wa mrado huo wa maji utarahisisha
shughuli nyingine
No comments:
Post a Comment