Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 22, 2015

WAKAZI WA CHUNYA WATAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU

.Inline image
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Elias John Tarimo akizindua Mradi wa Kisima cha Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.Inline image
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya


Wananchi wa kata ya Ngwala wilayani Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kutunza miundo mbinu inayojengwa katika kata yao hasa miradi ya maji ili waepukane na adha mbalimbali za kurudi katika adha walizokuwa wakipata mwanzo.

Haya yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Chunya Elias John Tarimo akiwa Mgeni rasmi wakati akizindua visima viwili vilivyojengwa na kampuni ya peak Resource limited ambayo hujihusisha na utafiti wa madini adimu chini ya ardhi yanayopatikana katika kata  ya ngwala wilayanii chunya mkoani mbeya  ambayo hutumika kutengenezea sumaku,mota,compyuta umeme wa sumaku,simu ambayo kwa tanzania tanapatikana wilaya ya Chunya pekee.

Tarimo alisema wananchi hawana budi kutunza miundo mbinu hiyo waliojengewa kwani wakiiharibu watarudi katika adha ya shida ya maji walikuwanayo hapo awali na kwamba waendeleze ushirikiano bora na kampuni hiyo kwani mahusiona mema ndiyo chanzo cha mafanikio ya kupata maendeleo katika kata yao.

Akisoma tarifa fupi ya ujenzi wa miradi mbalimbali waliojenga katika kata hiyo  meneja mradi wa Peak Resource limited Patrick Ochieng alisema miradi waliojenga ni visima viwili vilivyogharimu  milioni 16kila kimoja unjezi wa nyumba ya mwalimu iliyogharimu shilingi milioni 55 na ujenzi wa eneo la kupumzikia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Ngwala iliyogharimu  shilingi milioni  7 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 94.

Ochieng alindelea kueleza kuwa kwa sasa Kampuni yao ipo katika hatua za mwisho za utafiti na kwamba wanafwatilia leseni ya uchimbaji madini na kibali kutoka nemki ili kuanza uzalishaji na kwamba mgodi huo unauwezo wa kudumu kuchimbwa kwa miaka 40.

Aidha baadhi ya waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa miradi ni pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha  Neston Simoni na Diwani wa Kata ya Ngwala Donard Maganga ambao walisema wamefurahishwa na kile kinachofanywa na kampuni hiyo kwani wanajenga miradi bora kwa kutumia gharama nafuu.

Maganga aliwataka wakazi wa Ngwala kuiga mfano wa kampuni hiyo kwani nalisema nyumba waliojenga ya shilingi milioni 55 ukiweka Mkandarasi wangeweza kujenga kwa shilingi milioni 100 hivyo alisema mfano wa kampuni hiyo unapaswa kuigwa ili kuondoa ufisadi katika jamii yetu.

Kwaupande wa wananchi waliokuwepo hapo walishukuru kampuni hiyo kwa kupunguza adha walizokuwa nazo katika Kata yao kwani kwasasa wamekuwa na matumaini wa kupata walimu ambao watafundisha watoto wao katika mazingira yalio bora kutokana na uwepo wa nyumba bora ya Mwalimu ukilinganisha na hapo awali walikuwa wanakosa eneo la kujihifadhi,alisema Raisoni George.

Vile vile Elizabeti Yusuph mkazi wa ngwala alisema wao kama wakinamama walikuwa wachelewa kufanya shughuli za shambani kutokana na kufwata maji umbali mrefu kwani kutokana na uwepo wa mrado huo wa maji utarahisisha shughuli nyingine

No comments: