Baadhi ya viongozi wa Shiviwaka wakiwa kwenye mafunzo |
Baadhi ya Wandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mafunzo |
Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye picha ya pamoja. |
SHIRIKISHO
la Vikundi vya wakulima wa Kahawa Tanzania lenye makao makuu Mkoa wa
Mbeya (SHIVIWAKA) limeiomba Serikali kuondoa mlundikano wa kodi katika
zao la kahawa.
Rai hiyo ilitolewa
hivi karibuni na Mwenyekiti wa SHIVIWAKA,
Edward Masawe wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kubadilishana
uzoefu katika masuala ya utwala bora na uwajibikaji baina ya uongozi wa
shirikisho hilo na waandishi wa habari mkoani Mbeya.
Massawe
alisema hivi sasa kuna zaidi ya kodi tatu ambazo mkulima hulipa moja kwa moja
tangu kuanza kuotesha miche hadi mavuno jambo ambalo halisaidii kuinua uchumi
wa Mkulima wa Kahawa nchini.
Alizitaja
kodi hizo kuwa ni mchngo wa utafiti ambao mkulima hukatwa asilimia 0.75 ya dola
kwa kilo moja kwa mwaka wakati wa mavuno kulingana
na soko lililopo mnadani.
Alisema
tozo nyingine ni changizo la ushuru wa kila Halmashauri zinazolima zao la Kahawa
ambapo mkulima huchangia asilimia 5 ya bei iliyopo mnadani.
Mwenyekiti
huyo alisema kodi ya tatu ni changizo la maendeleo ya kahawa ambayo ilibuniwa na kusimamiwa na bodiya
kahawa kwa ajili ya pembejeo lakini badala yake fedha hizo huishia kwenye posho
za vikao vya bodi.
Aliongeza
kuwa malipo mengine ni gharama za magunia ya kusafirishia kahawa nje ya nchi ambayo
ni dola 2.5 kwa kila gunia hivyo kumfanya mkulima kushindwa kuuza kahawa yake
nje ya Nchi.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa SHIVIWAKA, Rabon Mbegunyingine njema alisema wakulima
wadogo wa zao la kahawa wamekuwa wakinyonywa kwa muda mrefu kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu
stahiki juu ya uhakika wa soko pamoja na bei elekezi hivyo umefika wakati sasa
serikali ikaingilia kati suala hilo .
Mwenyekiti
huyo amebainisha wazi kuwa endapo serikali itaamua kuingia kati na kuzungumza moja
kwa moja wakulima hao kutasaidia kuibua na kufahamu changamoto wanazo
kutana nazo badala ya kuiachia jukumu hilo bodi ya kahawa ambao nao
wamekuwa kikwazo kwa wakulima hao.
Aidha
mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo ya SHIVIWAHAKA ambaye pia ni katibu wa
Muungano group kutoka Utengule –Usongwe, Zakaria Mwashitete, alisema mkulima
anapewa fedha kidogo tofauti na bei inayokuwepo sokoni.
Alisema changamoto
hiyo inatokana na baadhi ya wajumbe wa bodi ya kahawa kumiliki makampuni ya
kununulia kahawa hivyo kujipangia bei.
No comments:
Post a Comment