Maandamano kuelekea katika Ukumbi ambapo vijana wanakutana kwa ajili ya Sherehe yao
Baadhi ya Vijana wakiwa katika Sherehe hiyo ya Vijana
Muwezeshaji wa Sherehe hiyo ya Vijana Mwadawa Mbando akiendelea kutoa utaratibu
Mratibu wa Mradi wa Restless Fadhiri Mtanga akitoa mada kuhusu Maendeleo ya Vijana
Wakili Stephen John akiwashauri vijana kuto tumika na wanasiasa
Vijana wakisikiliza kwa makini watoa mada kaika sherehe hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mzumbe Mbeya
Mmoja wa vijana kulia akipokea zawadi baada ya kupokea zawadi
William Otuku akitoa Maada kuhusu afya ya Uzazi kwa vijana
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Vijana Halmashauri jiji la Mbeya Onah Temu akitoa hotuba katika siku ya Vijana Duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya ilifanyikia Ukumbi wa Chuo kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
Picha ya pamoja
KATIKA maadhimisho ya siku ya
Vijana duniani yaliyofanyika Kimkoa katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Mzumbe
Kampasi ya Mbeya, Vijana wamekumbushwa kuhusiana na afya ya uzazi kwa vijana
pamoja na maendeleo yao.
Aidha katika kongamano hilo
ambalo liliandaliwa na mashirika binafsi ya Restless Developmentna Young &
alive initiative ambalo lilihudhuriwa na Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu na shule
za Sekondari za Jiji la Mbeya.
Akizungumza katika kongamano
hilo mwakilishi wa Shirika la Young & Alive Initiative, William Otuku,
alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwakumbusha vijana kuhusiana na maswala
yanayohusu afya ya uzazi kwa vijana ili waweze kuwa na uwezo wa kushiriki shughuli
za maendeleo wakiwa salama.
Aliongeza kuwa kauli mbiu ya
siku hiyo ni kuhakikisha vijana wanashirikishwa na kuhusishwa katika kupanga maamuzi mbali mbali hivyo hayo
yote yanaweza kutimia endapo wataelimishwa kuhusiana na afya ya Uzazi ili waliomashuleni
waendelee kufanya vizuri na kusaidia kutoa elimu kwa ambao hawako mashuleni.
“Vijana tunawapa elimuya
afya ya uzazi ili waweze kuwa imara
katika kushiriki shughuli za maendeleo za kijamii pamoja na kuwaepusha na
vitendo ambavyo vitaweza kuwaondolea katika hatari ya kupata magonjwa
yanayoweza kuepukika” alisema Otuku.
Kwa upande wake Mratibu wa
Mradi wa Shirika la Restless
Development,Fadhili Mtanga, alisema lengo la kongamano hilo ni kujadiliana kwa
pamoja kuhusiana na changamoto ambazo zinawakabili vijana pamoja na
kubadilishana mawazo juu ya kuweza kutatua na kukabiliana na vikwazo vya
maendeleo kwa vijana.
Alisema lengo la kuwahusisha
wanafunzi ni kutokana na kuwa na kundi kubwa la vijana wanaoanzia umri kati ya
miaka 15 hadi 35 ambao ni kundi kubwa katika jamii hivyo ni rahisi kwao
kupeleka mabadiliko kwa wananchi wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria
kongamano hilo.
“Sisi tumewalenga zaidi vijana
ambao ni wanafunzi kwa sababu tunaamini wanakubalika kaika jamii na nirahisi
kwao kutoa elimu ambayo iaweza kuwafikia wahusika kwa haraka zaidi” alisema
Mtanga.
Naye Mgeni rasmi katika
Kongamano hilo, Afisa Vijana wa Jiji la Mbeya, Ona Temu kutoka Ofisi ya
Maendeleo ya Jamii Jiji la Mbeya, alipongeza kwa wadau kujitokeza na kuandaa
kongamano hilo kwa kutambua mchango wa vijana katika jamii.
Alisema vijana wanapaswa
kuutumia vizuri umri kati ya miaka 18 hadi 40 kwa kujenga na kutafuta uchumi
ili kipindi cha miaka 40 hadi 60 anabaki kuwa msimamizi wa shughuli ambazo
alizifanyia kazi kipindi cha ujana wake.
Aliongeza kuwa kipindi cha umri
wa zaidi ya miaka 60 ni muda wa kufaidi matunda na kupumzika kwani utakuwa
tayari umeshafanya kazi ya kutafuta na kuzisimamia vizuri kwa malengo makubwa.
No comments:
Post a Comment