KATIKA kuhakikisha Wakulima
wanaondokana na kilimo cha mazoea, Taasisi ya Kilawa Enterprises ya mkoani
Mbeya imejikita katika utoaji wa elimu juu ya matumizi sahihi ya pembejeo za
kisasa kwa kilimo bora.
Wito huo ulitolewa na Meneja
Masoko wa Taasisi hiyo, Award Mpandila alipokuwa akitoa elimu kwa wakulima
waliotembelea banda lao katika maonesho ya wakulima nanenane yaliyomalizika
hivi karibuni ambapo alisema lengo la Taasisi hiyo ni kumsaidia mkulima wa hali
ya chini aweze kuongeza uzalishaji kwa kufuata kanuni bora za kilimo.
Alisema wakulima hufundishwa
mambo mbali mbali yakiwemo namna ya kuandaa shamba mapema kabla ya mvua za
kwanza kunyesha kuanziua mwezi Septemba na Oktoba na kasha kupanda baada ya
mvua kunyesha mwezi Oktoba na Novemba.
Alisema elimu nyingine
wanayompatia mkulima ni pamoja na kupanda kwa kutumia mvua za kwanza, matumizi
ya mbegu bora, upandaji wa nafasi kwa kutumia vipimo sahihi na matumizi ya
mbolea ili kupata mavuno mengi.
Mpandila alisema wakulima hao
wakipata elimu hiyo sambamba na kukumbushwa palizi kwa ajili ya kuondoa magugu
mashambani kulingana na aina ya mazao pamoja na kuzuia wadudu waharibifu pamoja
na magonjwa mbali mbali yanayoharibu mazao.
Aliongeza kuwa pamoja na elimu
hiyo bado wakulima wanatatizo la kutowahi kuvuna mazao yao mara baada ya
kukomaa jambo linalopelekea upotevu wa mazao mashambani ambapo pia hufundishwa
namna ya kuhifadjhi ghalani na kuanza kusafisha shamba kabla ya msimu wa kilimo
kuanza.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment