Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 11, 2015

WAZIRI MKUU PINDA ALIPOFUNGA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI‏

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa hotuba ya kufunga maonesho ya wakulima nanenane 2015 Kanda ya Nyanda za juu kusini.
 Meneja wa Uwanja wa John Mwakangale, Mwakibete Kasilati akitoa taarifa ya hali ya uwanja kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
 Meneja wa Uwanja wa John Mwakangale, Mwakibete Kasilati akitoa taarifa ya hali ya uwanja kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Bwana shamba wa Balton alipotembelea banda lao.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mfugaji wa nyuki ambapo alielezwa kuwa kwa sasa kuna mwamko mkubwa wa ufugaji wa nyuki kwa njia za kisasa.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokea zawadi  kutoka katika banda la Mlele.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na baadhi ya Wakuu wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini wakipata maelezo kutoka katika kipando cha Mpunga kilichopo kwenye banda la Wilaya ya Tunduru.
 Waziri Mkuu Pinda akimuangalia Mbuzi bora wa maziwa.
 Waziri Mkuu Pinda akiwa sambamba na mke wake Mama Tunu Pinda wakiangalia bidhaa mbali mbali katika mabanda.
 Waziri Mkuu Pinda akimwelekeza tofauti ya asali Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akibadilishana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Sad Mwambungu.

 Mke wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda akiwea ameshika parachichi.
 Band ya Baby Tot ikitoa burudani katika kilele cha nanenane.
 Kikundi cha nyimbo za kisafwa wakitoa burudani.
 Baadhi ya wakulima na waoneshaji wakiwa jukwaani tayari kumsikiliza Waziri Mkuu akifunga maonesho ya nanenane.
 Mwenyekiti wa Mviwata Mkoa wa Rukwa akisoma risala kwa niaba ya wakulima.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoroi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi Waziri Mkuu.
  Mama Tunu Pinda akiwasalimia wakulima na wananchi.
Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akitoa hotuba fupi ya kuwasalimia wananchi.
 Makamu Mwenyekiti wa TASO Kanda Crispin Mtono akitoa maelezo mafupi kwa wakulima.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewaagiza Wakuu wa Mikoa na wakuu wa Idara kuhakikisha wanawaandaa washiriki wa maonesho ya wakulima mwaka huu kuonesha kile walichojifunza katika maonesho yajayo.
Waziri mkuu alitoa agizo hilo  alipokuwa akifunga maonesho ya sikukuu ya wakulima nanenane katika mikoa ya Nyanda za juu kusini yaliyofanyika mkoani Mbeya ambapo alisema Sikukuu hizo ni sawa na shule hivyo lazima washiriki waseme walichojifunza.



Alisema ili malengo yaweze kutimia ni lazima kuwepo na utaratibu katika maonesho yajayo kwa wakulima na waoneshaji kusema katika maonesho yaliyopita walijifunza nini na wao wamekuja na kipi kipya hali itakayochangia kuleta maana halisi ya siku hiyo.
“Ni vizuri tukawa na utaratibu hata wa dakika kumi tu mkawachagua hata wawakilishi wachache wakatueleza katika maonesho yaliyopita walijifunza nini na hivi leo wamekuja na teknolojia zipi, kwani haya maonesho kwangu mimi ni shamba darasa pia ni shule lazima tuelezane” alisema Pinda.
Aliongeza kuwa kama nguvu kubwa itaendelea kuelekezwa kwenye sekta ya kilimo na mifugo itasaidia sana katika kukuza uchumi wa Nchi kwani sekta hiyo inawagusa zaidi watu wa chini na maskini ambao shughuli zao kubwa ni kilimo na mifugo.
Alisema hata uongozi ujao unapaswa kuhakikisha suala la kilimo linapewa kipaumbele kwani Taifa lolote linahitaji kuwa na chakula cha kutosha ili liweze kujiendesha ndipo shughuli zingine za kiuchumi zinaweza kusonga mbele lakini kukosa chakula kunakuwa ni aibu kwa Nchi.
“Taifa lisiloweza kujilisha ni aibu siku zote hivyo hakuna sababu ya Tanzania kufikia huko kitu muhimu katika maisha ni chakula hata ndani kukiwa na chakula kunakuwa na amani mi nafikiri haya uongozi ujao utayazingatia haya” alisema Waziri Mkuu.
Alisema hivi sasa Tanzania iko miongoni mwa Nchi 20 Duniani ambazo uchumi wake unakua lakini utafiti unaonesha kuwa wananchi wengi bado ni maskini jambo lililoelezwa kuwa uchumi unategemewa na vyanzo vichache ambavyo ni Nishati, madini na utalii vitu ambavyo mtu wa chini hana uwezo navyo.
Aliongeza kuwa ili kuinua uchumi wa Tanzania na kuhakikisha tofauti kati ya walionacho na wasionacho inapunguzwa kwa kuwafikia watu wa chini na kuendeleza kile wanachojishughulisha nacho ili kiwe kibiashara na hatimaye kumuingizia kipato.
Kwa upande wa maonesho ya mwaka huu, Waziri Mkuu alisema ameona mabadiliko hasa katika kuongeza thamani ya mazao na usindikaji hususani kwenye vifungashio vyenye ubora utakaorahisisha upatikanaji wa masoko popote duniani.

“Nisema kwamba nimetembelea maonesho sehemu mbali mbali na hapa nimepitia mabanda machache nimeona utofauti kwani maeneo ya mpunga yameonesha juhudi nzuri katika kusindika kupanga madaraja na kufunga kwa vifungashio vizuri sambamba na korosho” alisema Pinda.
Aliongeza kuwa jambo lingine alilofarijika nalo katika maonesho hayo ni pamoja na uwepo wa Taasisi ya kilimo cha mboga mboga na matunda(TAHA) katika mikoa ya nyanda za juu kusini kutasaidia kilimo hicho kwani Mikoa hiyo inauwezo wa kulima isipokuwa walikuwa wanakosekana wataalamu.
Alisema jambo lingine ni kundi la vijana kuingia katika sekta ya kilimo na mifugo jambo ambalo litasaidia kuinua sekta hiyo kutokana na matumizi mazuri ya elimu zao,na kuoneza kuwa katika uongozi wake anajivunia kuacha neema ya chakula katika kipindi ambacho anaondoka madarakani.
NA MBEYA YETU                                                                                                                         

No comments: