Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 27, 2015

WATIA NIA UDIWANI KATA YA MAENDELEO JIJINI MBEYA WAELEZA VIPAUMBELE VYAO WAKIJINADI KWA WAPIGA KURA.

 Mwenyekitiwa CCM Kata ya maendeleo akiwaongoza viongozi wa Kata hiyo kuimba wimbo
 maalum wa Chama wakati wa kampeni ya kuwanadi watia nia ya kugombea Udiwani.
 Mtia nia ya Udiwani, Peniel Mwaisango akijinadi mbele ya wanachama wa CCM Kata ya Maendeleo.
 Mgombea Juma Kilongola akimwaga sera.
 Modest Shiyo ambaye anatetea nafasi yake akijaribu kuwashawishi wapiga kura ili aendelee kuwawakilisha.
 Mtawa Kapalata Mwaijumba akitoa sera zake na kuwashawishi wapiga kura.
 Katibu wa CCM Kata ya Maendeleo, Isaya Mwakibuti akiwaonya wagombea kuhusu kufanya siasa za kuchafuana.
Baadhi ya Wanachama wakiwasikiliza watia nia

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Maendeleo jijini Mbeya, Bonifasi Kasyunguti amewataka wanachama wote wa Chama hicho kuhakikisha wana vitambulisho vya
kupigia kura pamoja na Kadi za Chama ndipo watakaporuhusiwa  kupiga kura za maoni.
Mwenyekiti huyo aliyasema hayo jana katika mkutano wa Hadhara wa Watia nia ya kugombea kuteuliwa na Chama kwa
ajili ya kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya udiwani wa Kata ya Maendeleo iliyopo jijini Mbeya kuomba ridhaa
kutoka kwa wanachama. 

Alisema katika kampeni baadhi ya wagombea wanawanunulia Kadi wanachama ili kuwashawishi kuwapigia kura wakati wa Kura za maoni ndani ya Chama na kusahau kama wanazokadi za kupigia Kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha alitoa wito kwa Makatibu wa Matawi kuwachunguza na kuwafuatilia wale wote wanaouza kadi kuholela nje ya utaratibu wa Chama na kwamba kadi zote zinatolewa na kuuzwa na
katibu ambaye pia huwasajili katika daftari maalum litakalotumika wakati wa kupiga kura.
Aliongeza kura Kura za maoni zitapigwa Agost mosi mwaka huu kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni ambapo wapiga kura wote ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi majina yao yatabandikwa katika mbao za vituo
vya kuoigia kura.
Katika Kampeni hizo zilizokuwa na wagombea wanne wanaowania kuteuliwa na Chama hicho walipata nafasi ya kueleza vipaumbele vyao kwa wananchi wa Kata ya Maendeleo
endapo watateuliwa na kufanikiwa kuwa madiwani.
Wa kwanza kujinadi alikuwa ni Mtawa Kapalata Mwaijumba
(56) ambaye alisema endapo atafanikiwa kuwa diwani ataweza kushughulikia mgogoro wa makazi na nyumba, mipaka kati ya Kata ya Maendeleo na majirani pamoja na suala la miundombinu ya Barabara.
Mtia nia wa pili alikuwa ni Modest Shiyo ambaye anatetea nafasi yake ambapo alitumia muda huo kuwaeleza wanachama kuwa katika kipindi cha miaka mitano ametekeleza ahadi
nyingi
zikiwemo ujenzi wa Daraja, Barabara za lami, na barabara za ndani ya Kata pamoja na ushirikiano ndani ya wananchi na
kwamba akichaguliwa tena atakamilisha maeneo yaliyobaki.
Kwa upande wake mtia nia wa tatu Juma Kilongolo aliomba wanachama kumpitisha kwani anao uwezo wa kusambaratisha kambi za upinzani na hatimaye kufanikiwa kuwa Mbunge na kuwawakilisha wananchi wa Kata ya Maendeleo.
Naye mtia nia wa Mwisho, Peniel Mwaisango alisema
endapo atafanikiwa kuingia katika
Baraza la madiwani la Jiji atahakikisha vitega uchumi vilivyomo ndani ya Kata kunakuwa na asalimia chache ya mapato yakayobaki kwenye kata ili kusaidia shughuli za maendeleo
kwa kumshawishi Mkurugenzi na Baraza la Madiwani.
Alivitaja vitega uchumi hivyo kuwa ni pamoja na ukumbi wa Mikutano wa Mkapa ambao upo katika Kata hiyo lakini wananchi hawafaidi na fedha zinazotokana na shughuli
zinazofanyika ndani ya ukumbi huo kila siku.
Mbali na hilo Mwaisango alisema katika sekta ya michezo atajikita katika kuinua soka la watoto ili kuwaepusha kujiingi
za katika vitendo vya kihalifu kwa kukarabati uwanja
wa mpira na kununua vifaa vya michezo pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara na taa za mitaani ili mji uwe
mzuri.
Na Mbeya yetu

No comments: