|
Mwonekano wa Ajali hiyo |
|
Gari Ndogo ambayo ni IT ikiwa pembeni mara baada ya kungoga Noah kwa nyuma. |
|
Polisi wa Usalama Barabarani wakiwa katika eneo la tukio mara baada ya Ajali hiyo kutokea |
|
Abilia
waliokuwa kwenye basi la Al saedy wakiwa na mizigo yao mara baaada ya
ajali hiyo kutokea Maeneo ya mama john jijini Mbeya leo asubuhi. |
|
Mwonekano
wa Gari ndogo aina ya Noah ambayo imegongwa na Basi la kampuni ya Al
saedy ikiwa inavutwa na gari ya Polisi.(Picha na David Nyembe wa Fahari
News) |
Ajali
mbaya imetokea asubuhi ya leo jijini Mbeya baada ya magari matatu kugongana
katika eneo la Mama John ambapo magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi
la Al Saedy linalofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda mkoani Dar es Salaam,
Noah na gari lingine dogo (IT) Ajali hiyo imetokea wakati dereva ambaye
hajafahamika kwa jina mara moja wa basi la Al Saedy lenye namba za usajili T
T830 BQG lililokuwa limetokea kituo kikuu cha mabasi jijini Mbeya kuelekea Dar
es Salaam alipokuwa akitaka kulipitagari dogo katika eneo hilo ambapo akakutana
uso kwa uso na gari dogo aina ya Noah lenye namba za usajili T 969 BWG
lililokuwa likitokea Uyole na likiwa na watu watano walionusurika kifo.
Taarifa za mashuhuda kutoka eneo la tukio
zinasema kuwa baada ya Basi hilo la abiria kugongana na Noah gari lingine dogo
IT lililokuwa likielekea Tunduma kutoka Dar es Salaam liligonga Noah upande wa
nyuma. Kutokana na kilichoshuhudiwa katika eneo la ajali, mashuhuda
vwametanabaisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na kutokuwa makini kwa
dereva wa basi hilo ambalo abiria wake wote wamenusurika kujeruhiwa.
Aidha ajali hiyo imesababisha majeraha makubwa
kwa dereva wa Noah ambaye amevunjika mguu wake pamoja na dereva wa gari dogo IT
ambao wote waliwahishwa hospitalini kupatiwa huduma ya kwanza (wote
hawakufahamika majina yao mara moja). Hakuna vifo katika ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment