Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 27, 2015

HENRY HARRISON MWANGAMBAKU AWANIA UDIWANI KATA YA FOREST JIJINI MBEYA KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA


Habari za leo ndugu zangu na wananchi wote wa forest.

Naitwa Henry Harrison Mwangambaku. Kijana niliyezaliwa forest miaka 32 iliyopita. Nina familia ya mke na watoto wawili.

Baada ya kupata elimu ya msingi katika shule ya muungano. Nilijiunga na shule ya secondary, Mbalizi, na baadae Galanos, Jitegemee na hatimaye kuhitimu chuo kikuu cha Dar es salaam (Udsm) katika shahada ya kwanza ya fani ya Baishara yaani (bachelor of Commerce and management in accounting.)

Leo hii tarehe 25 July 2015. Nakuja mbele yenu wananchi wa forest.

Nikiwa na jambo moja ambalo ni kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kuwa mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya forest. Kupitia cha cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Wengi wetu watajiuliza kwa nini nimeamua kufanya hivi.

Kwanza kabisa niseme kwamba ninatumia haki yangu ya msingi ya ki katiba kama mwana Chama wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivyo ninahaki za kimsingi za kuomba kuchaguliwa kuwa muwakilishi wa kata hii muhimu kabisa katika maendeleo ya jiji la Mbeya.
Nipo tayari kuzisogeza fursa zilizopo kwa ajiri ya wana forest. Ambazo zinaweza kupatikana kutoka sehemu zifuatazo.

KWANZA, ni fursa ya mikopo ya wanawake na vijana ambayo hutolewa kwa vikundi vya maendeleo.mikopo hiyo inatokana na 5% ya mapato ya ndani ya jiji la mbeya ya kila mwaka
PILI, ni taasisi zilizopo forest mfano BOT, Mzumbe University na Ofisi za police mkoa, Mahakama kuu, na wawekezaji wakubwa waliopo katika kata ya forest. Ambao kwa nyakati tofauti wameonyesha utayari wa kuwasaidia wananchi wa forest hususani vijana kupitia michezo.

TATU, ni utayari wa kasimamia mazingira na taasisi zake, Kwa weredi wa hali ya juu, Kwa kuviunga mkono vikundi na taasisi mbali mbali zitakazojitolea kuifanya kata ya forest kuwa namba moja kwa usafi mkoa wa Mbeya.

Kusudi tuweze kunufaika na fursa hizi. Tunaitaji kuwa na kiongozi(mgombea) mwenye sifa zifuatazo.
1.Anayeweza kujitolea kwa mali,akiri na mda wake kwa ajiri ya wananchi forest.

2.Mwenye kujua umuhimu wa kuwatumikia na kuwahudumia wananchi wake.

3.Anayejumuika na  wananchi wake wakati wa shida na dharula mbali mbali kama misiba
, na kutambua watu au jamii zinazoitaji misaada ya kijamii.


Kimsingi hii sio kazi rahisi lakini ni kwamba....

NIMEJIPIMA, NIMETAFAKARI KWA KINA NA NIKO TAYARI KUWATUMIKIA WANANCHI WA FOREST. 

*****NATANGAZA NIA****



Nawaomba wananchi wote wa forest kuniunga mkono katika juhudi zangu za kuwatumikia wanaforest. Asanteni.

No comments: