Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, July 29, 2015

NYENYEMBE AKANA KUTIMKIA ACT-WAZALENDO

MWANDISHI wahabari  mkongwe na Mwakilishi wa Kampuniya Free Media nyanda
zajuukusini,Christopher Nyenyembe aliyejitosa kuwaniaUbunge jimbo la Mbeya mjini (Chadema)nakushindwa kwenye kura za awali za maoni zilizompa ushindi,JosephMbilinyi(MrSugu) amekana kutaka kutimkia chama kipya cha ACT-Wazalendo kinacho ongozwa na aliye kuwa naibu katibu Mkuu 
chadema Zito kabwe.
Habari za kuaminika ambazo Gazeti hili limezinasa  kuwa,Nyenyembe ambaye jina lake lilikuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa jiji  hilo na ndani ya Chadema kuwa ana mpango wa kuhamia chama kinacho  ongozwa na Zitto Kabwe kunatokana na mizengwe yahali ya juu iliyofanyika kwenye uchaguzi wakura zamaoni julai 22 mwaka huu kukiwemo madai ya  vitendo
vya rushwa
Nyenyembe aliyejitosa kwamara ya pili kugombea ubunge ametajwa na baadhi ya wanasia sana marafikizake wa karibu kuwa wanamshawishi kuhamia ACT-Wazalendo na kukiacha chama chake cha Chadema alichokitumikiakwa miaka 22 tangu alipojiunga mwaka  1993,taarifa hizo alizozitoa wakati alipokuwa akijinadi.
Kusambaa kwa taarifa hizo kulifanikisha kuwepo kwa mahojiano ya moja kwa moja
kati ya Waandishi wahabari na Nyenyembe mwenyewe ambaye kwa kauli yake alikanusha nakukiri wazi kuwa hanampango wowote wa kuhamia ACT-Wazalendo na kwamba huo ni 
uvumi na uzushi ulio onezwa na wana CCM.
“Sinampango wa kuhamia chama kingine,nimekuwepo Chadema kwa zaidi ya miaka 20 tangu nilipo pewa kadi ya kwanza naMarehemu Bob Makani mwaka 1993,siwezi kuondoka kirahisi namna hiyo,kura za maoni ndani ya chama changu ni za
awali,zilikuwa nzuri licha ya kukabiliwa na changamoto 
nyingi ambazo 
sina muda wakuzieleza” alisemaNyenyembe.
Alisema kuwa anajua  nafasi aliyonayo ndani ya chama chake ya kuwa mjumbe wakamati yautendaji ya jimbo la Mbeya mjini na kuwa mchango wake bado unathamaniwa ndani ya Chadema kuliko kwenda kwenye chama kingine ambacho itakuwa kazi kubwa  kujijenga kisiasa.
“Najua wapo watu wengi waliotamani kuniona nikiwa jukwaani kupeperusha benderaya Chadema,mchakato ulikuwa mgumu  hivyo sio jukumu langukufahamu nini kitaamuliwa kwenye vikao vyajuu  nasiwezi kuzungumzia rushwa kwakuwa sina ushahidi,wenye ushahidi  wawasilishe kwenye mamlaka za juu kwani hata chama chetu hakimtaki mgombea aliyetoa rushwa kupata ushindi” alisema mkongwe huyo wahabari.
Aliongeza kuwa kazi kubwa anayoweza kuifanya ni kuhakikisha kuwa anakisaidia
chama chake kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu dhidi ya CCM na kwenye mkoa wa Mbeya ataungana na mgombea yoyote jina lake  litakaloteuliwa ilikushinda viti vya ubunge katika majimbo yote na kata  zote za jiji la Mbeya ilikuongoza halmashauri.
Alisema kuwa yupo  tayari wakati wowote kuitumikia Chadema na kutumia taaluma yake ya  habari ana nafasi kubwa ya kutoa elimu ya uraia ili kuwajengea uwezo
wananchi ili kuchagua viongozi bora na wenye sifa ya kupiga vita vitendo vyote vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya wanasiasa.
“Sinampangowakutimkia ACT-Wazalendo wanaosema nataka kuhamia huko habari hizo sio za  kweli,naona kuna watu wanatamani sana niwe Mbunge wao kutokana na uwezo  mkubwa nilionao,chamachetu kina kazi nyingi za kufanya sio lazima niwe mbunge,siku ikifika nitakuwa, hivi sasa nina jukumu zito la kuungana nawana Chadema wenzangu ili tushinde na sivinginevyo” alisemaNyenyembe.
Na Mbeya yetu.

No comments: