Mbunge wa Ileje anayetetea nafasi yake, Aliko Kibona akizungumza na wananchi wa kata ya Luswisi hivi karibuni.
Mtangazaji wa TBC Mbeya Hosea Cheyo akitoa msaada wa fedha taslim kwa kikundi cha ngoma za asili wilayani Ileje.
Hosea Cheyo akiwa na mmoja wa wazee wa Kata ya Luswisi wilayani Ileje wakibadilishana mawazo.
Hosea Cheyo akiwa na baadhi ya wananchi wa Ileje wakiangalia burudani ya ngoma za asili.
Hosea Cheyo akiwa na viongozi wa kampuni ya Simu ya TTCL walivyotembelea Kata ya Luswisi.
MBUNGE wa Jimbo la Ileje anayetetea nafasi yake, Aliko Kibona, amewataka
wananchi wa jimbo hilo kumuongeza miaka
mingine mitano ili akamilishe miradi ya maendeleo aliyoianza.
Aliyabainisha hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na wapiga
kura kuhusu adhma yake yakutetea
nafasi ya ubunge.
Aidha Kibona amesema baada ya kumaliza miaka mitano atawaletea mtu ambaye yeye
anamuona anamapenzi mazuri na wakazi wa Ileje na anauwezo wa kurithi viatu
vyake endapo atashawishiwa kugombea kiti hicho mwaka 2010.
Aliko Kibona mbali na kuomba kuongezewa muda na kuaandalia mgombea wananchi wa
Ileje amepata upinzani mkali kutoka kwa wagombea wengine ambao ni Godfrey
Kasekenya,Janeth Mbene,Lyson Mnkondya,Willium Ndile na Marcelin Ndibwa.
Alisema miradi ambayo ameianza nab ado
kukamilika ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa nyumba za walimu ambazo amekuwa
akitafuta misaada kutoka kwa wadau wa
ndani na nje ili kuhakikisha walimu wanaishi katika mazingira mazuri ili
kuboresha sekta ya elimu.
Aliongeza kuwa mbali na sekta ya elimu pia suala la umeme vijijini lipo katika hali nzuri huku ujenzi wa barabara ya Lami
kutoka Mpemba hadi Isongole ikitarajiwa
kuanza muda wowote baada ya Waziri wa
Ujenzi Dk. John
Magufuli ambaye aliahidi kuijenga anakuwa Rais wa Jamhuri ya
Muunganowa
Tanzania hivyo akiingia Ikulu atakutana na ahadi hiyo.
Akizugumzia mtu anayedhani anaweza kumrithi ifikapo 2020,Kibona alimtaja
Mtangazaji na mwakilishi wa Shirika la
Utangazaji Tanzania(TBC)Mkoa wa Mbeya, Hoseah Cheyo.
Alisema katika vijana anaowaona wenye uchungu na Ileje ni Cheyo hivyo atatumia
muda mwingi kumshawishi na kuanza kumuandaa
katika chaguzi za ndani za chama kuanzia mwaka 2017.
Alisema Cheyo ni mchapa kazi kwani utendaji wake na jinsi anavyoripoti habari
za Ileje zinaonesha kuwa na kiu yakuona watu wa Ileje wakipata
maendeleo
ya haraka na kuwa Wilaya yenye mafanikio makubwa katika kipindi
kifupi.
“Niseme kutoka ndani ya mtima wa moyo wangu mtu pekee ninae muona anaweza
kunirithi ni Osea Cheyo, niko tayari kumshawishi na kuanza
kumuandaa
kuwa Mbunge kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama 2017”alisema Kibona.
Kwaupande wake Cheyo alipoulizwa utayari wake wa kushikaUbunge wa Ileje
alisema anashauku kubwa ya kuwaletea maendeleo watu wa Ileje hivyo
wakati ukifika atakuwa tayari kama itampendezaMungu.
Aliongeza kuwa anatamani Wilaya ya Ileje ikiwa ni kitovu cha kilimo cha Kahawa isiyotumia
madawa na mbolea za madukani hapa nchini na kuwa na wanunuzi kutoka pande zote
za dunia jambo litakalochangia kupatikana kwa
maendeleo haraka ikiwemo miundombinu.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment