WAZIRI wa Maliasili na utalii,Lazaro Nyalandu akiongea na waandishi wa habari wa mkoa Mbeya |
WAZIRI
wa Maliasili na utalii,Lazaro Nyalandu amewashukuru wanachama wa CCM Mkoa wa
Mbeya waliojitokeza kumdhamini katika harakati za kuwania kuteuliwa kugombea
urais.
Licha ya kuwashukuru wanachama hao lakini Waziri Nyalandu aligoma kutaja idadi ya wadhamini aliowapata na kudai kuwa atakachokiwasilisha makao makuu ya Chama ni Idadi ya wadhamini inayotakiwa.
Nyalandu aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake ya kutafuta wadhamini kutoka kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi ili aweze kuteuliwa kuipeperusha bendera katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ujao.
Alisema ndani ya CCM kuna Demokrasia kubwa hali iliyopelekea wanachama kujitokeza kwa wingi kutaka kugombea Urais lakini kikubwa ni kila mgombea kuweka maslahi ya Chama mbele ili kuimarisha umoja na mshikamano na kuwavutia walio nje ya Chama kujiunga nacho.
Aliongeza kuwa katika mchakato huo mwisho wa siku Chama kitamteua mtu mmoja atakayesimama na kupeperusha bendera katika uchaguzi huo hivyo wagombea wote watapaswa kumuunga mkono ili Chama kiweze kuibuka na usgindi mkubwa na kishindo.
Waziri
Nyalandu alisema katika kinyang’anyiro hicho amejifunza mambo mengi ambayo
yamemsukuma na yeye kuingia humo likiwemo kupanuka kwa demokrasia ndani ya
Chama na jinsi wanachama wengi walivyojitokeza kuichukua fomu za kuteuliwa
kugombea Urais.
Alisema
jambo lingine ni changamoto zinazowakabili wananchi wa kawaida pamoja na jinsi
Nchi ilivyopiga hatua katika maeneo mbali mbali chini ya uongozi wa Rais wa
awamu ya nne na kuongeza kuwa Rais ajaye hatakuwa na budi ya kufuata nyendo
zake katika uongozi wake.
Alisema kama akiteuliwa na kushinda Urais atahakikisha anawekeza katika rasilimali watu katika kuwawezesha kukabiliana na changamoto zinazojitokeza za wakati kwa kutumia fursa zilizopo pamoja na kuwezesha vijana ili waweze kulitumikia Taifa.
Kuhusu
idadi ya Wadhamini aliowapata katika ,ikoa yote aliyopita Nyalandu alisema
amebakiza mikoa mitatu ambayo lazima akamilishe lakini idadi ya wadhamini
amesema atawasilisha idadi inayotakiwa na Chama ya wadhamini 450 tu na
sio vinginevyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment