JUMLA ya watiania 26 kutoka jimbo la
Mbozi Mashariki wamerejesha fomu katika ofisi za Wilaya, kati 39 ambao
walijitokeza kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera cha chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kwa nafasi ya Ubunge katika uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Baada ya kurejesha fomu hizo baadhi ya wagombea walijinasibu kuwa wanauwezo wa
kutumikia jamii katika nafasi ya Ubunge endepo chama kitawapa ridhaaa ya
kupeperesha bendera kutoka na uwezo wao wa kujenga hoja na kulifahamu jimbo
hilo vizuri kutoka kuwa wazawa lakini pia wamekukitumikia chama hicho kwa muda
mrefu.
Abaraham Msyete ambaye ni mmoja
wawatiania alisema kutokana na kukitumia chama hicho kwa zaidi ya miaka
kumi,huku akifanya kazi mbalimbali za kukimarisha chama hivyo ameamua kuchukua
fomu na kuomba chama kiwezi kumpitisha kwani amejitafakari na kuona anaweza
kuwatumia wananchi wa Jimbo la Mbozi Mashariki na taifa kwa ujumla katika
nafasi ya Ubunge.
‘Nina ozeofu na jimbo hili na kwani
nimezaliwa Mbozi na kusoma Mbozi hivyo na pia nimeanza harakati za kukinadi
chama tangu nikiwa mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar-es-laamu, hivyo mpaka sasa
ni zaidi ya kumi nipo ndani ya Chadema ni imania yangu chama kitanipa ridhaa ya
kupeperusha bendera katika uchagu ujao’alisema Msyete
Mbali na hilo lakini Msyete
alibainisha baadhi ya Mambo kumi ambayo anayapa kipaumbele ambavyo atapaswa
kuyatekekeleza mara tu atakuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Msyete alisema kuwa baadhi yake
ni uboreshaji wa kilimo chenye tija,miondombinu ya barabara,maji,ajira
kwa vijana,elimu,wa huduma afya pamoja na kupiginia haki kwa wakulima.
Katika sekta ya elimu Msyete alisema
kuwa Wilaya Mbozi yenye wakazi zaidi ya 490,000/ na shule nyingi za msingi na
Sekondari lakini hakuna chuo cha ufundi hata kimoja ambacho kingeweza kuwaanda
vijana kuwa mafundi ambayo ni fursa pekee kwao kuweza kuji ajiri.
Kwa upande wake Stephen Mwamengo
alisema Mbozi,inakabiliwa na na matatizo mengi tangu kupata Uhuru na hilo ndiyo
yaliyo msukumwa kuchukua fomu na kuomba ridhaa kupitia chama chake kiwezo
kupitisjha ili awe mgombea Ubunge.
Alisema kuwa jimbo la Mbozi
Mashariki limejaliwa rasilimali nyingi ikiwemo ardhi yenye rutuba lakini
viongozi waliotangulia katika awamu zote hawajaweza kuwasadia wananchi
kuondokana na umasimni kutoka na ardhi hiyo.
Alisema kuwa endapo atachaguliwa
hatau ya kwaza ni kuwapigia wananchi wawezi kutambua umuhimu wa ardhi wanayo
miliki na ili kuweza kapata hata mikopo katika taasisi za fedha ili kupata
mikopo.
Hata hivyo katika jimbo hilo la
Mbozi Mashariki kumekuwa na sitofahamu kutoka na watia nia hao kuchukua na
kurejesha fumu zao katika ofisi mbili tofauti huku kila upande ukidai kuwa
unahaki ya kulisimamia zoezi huku kiloa upande ukisema kuwa Ofisi zao ni za
Wilaya.
Katika ofisi ya kwanza ambayo
msimamizi wa zoezi la kuchukua na urejeshaji wa fomu ni Michael Mwamlima ambaye
ni katibu wa Bavicha, amabaye aliieleza Tanzania Daima kuwa kuwa katika ofisi
hiyo watia nia walikuwa nane na wote walichukua fomu na wato nane ndiyo walio
zirejesha.
Aidha katika ofisi nyingine ambayo
msimamizi wa zoezi hilo,Osward Mweluka ambaye alijinasibu kuwa ni kaimu Katibu
wa chama hicho ngazi ya Wilaya ya Mbozi alisema katika ofisi hiyo watia nia
walikuwa 29 walio chukua fomu ni 18 na ndiyo walio rejesha.
|
No comments:
Post a Comment