Semina ikiendelea
Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Mbeya, Enock
Nyasebwa akifungua mafunzo kuhusu lishe bora.
Wakiendelea na semina huku wakifuatilia kwa makini
Mkurugenzi wa shirika la Land O Lakes linalojishughulisha na
utoaji wa elimu kuhusu lishe bora, Dk. Rose Kingamkono, akizungumza na
waandishi wa habari
Maelezo yakiendelea
WANANCHI wa Mikoa ya Iringa na Mbeya wametakiwa kuacha kutumia chakula cha aina moja na badala yake wazingatie kanuni za lishe bora ili kuepukana na tatizo la utapiamlo.
Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Land O Lakes linalojishughulisha na utoaji wa elimu kuhusu lishe bora, Dk. Rose Kingamkono, katika semina kwa waratibu wa Afya wa Wilaya za Mikoa ya Mbeya na Iringa iliyofanyika jana Uyole jijini Mbeya.
Dk. Kingamkono alisema licha ya mikoa ya Mbeya na Iringa kuongoza katika uzalishaji wa mazao ya chakula lakini wananchi wake wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa utapiamlo unaosababishwa na ukosefu wa lishe bora.
Alisema changamoto kubwa iliyobainika ni kwamba wananchi hao wengi wanalima mazao kwa ajili ya biashara na hivyo kukosa utamaduni wa kubakiza kwa ajili ya chakula na namna ya kupangilia lishe bora kwa kubadilisha aina ya vyakula.
Alisema kitendo cha ukosefu wa lishe bora kwa wananchi kunazoilotesha hali ya uchumi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kutokana na ugonjwa wa utapiamlo ambao huathiri nguvu kazi na kupelekea taifa kuendelea kuwa maskini.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku tano kuanzia Juni 23 hadi Juni 26, mwaka huu walisema sababu kubwa ya kuwa na utapiamlo katika Mikoa hiyo ni kutokana na mila na desturi miongoni mwa jamii.
Afisa kilimo Wilaya ya Mbarali, Mary Nyika alisema tatizo kubwa ni mazoea pamoja na mila na desturi na mitazamo potofu juu ya lishe bora iliyojengeka katika jamii kwa kula aina moja ya chakula pamoja na kuuza mazao yakiwa bado mashambani.
Alisema baada ya mafunzo hayo wanatarajia kuanza kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupangilia vyakula vyenye lishe ili kupunguza tatizo la utapiamlo lililopo hivi sasa.
Kwa upande wake mgeni rasmi wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Katibu tawala msaidizi Mkoa wa Mbeya idara ya Kilimo, Enock Nyasebwa aliwataka waratibu wa afya baada ya mafunzo hayo kuja na mapendekezo juu ya nini kifanyike ili kupunguza tatizo la utapiamlo katika jamii.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment