WAZIRI wa ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela(CCM) amewapongeza
wakazi wa kyela kwa ushirikiano.
Dk. Mwakyembe alitoa pongezi hizo kufuatia umati mkubwa wa Wananchi kujitokeza katika
mazishi ya kaka yake
Christian Mwakyembe aliyefariki dunia akiwa anatibiwa nchini
India na kuzikwa kijijini kwao Ikolo
wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Akizungumza kwa niaba ya familia ya
Mwakyembe, Dk. Mwakyembe alisema ushirikiano uliooneshwa na wananchi wa Kyela na Watanzania
kwa ujumla tangu msiba ukiwa Dar es
salaam, Mbeya mjini na hatimaye kijijini kwao ni mkubwa sana na unapaswa kupongezwa.
“Sisi kama familia hatuna cha kuwalipa
zaidi ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu kwani mlikuwa nasi tangu
mliposikia Kaka yetu amefariki kule India alipoletwa Dar es
salaam, kule Mbeya na hapa kijijini
Kwetu tunashukuru sana” alisema Dk. Mwakyembe.
Hata hivyo shughuli za msiba huo
zilibebwa na Chama cha waandishi wa habari za uwekezaji na utalii(TAJATI) chenye makao
makuu jijini Mbeya kufuatia mmoja wa
wafiwa ni mwanachama wa chama hicho.
Mwanachama huyo Felix Mwakyembe ambaye
ni mdogo wa Marehemu alipongeza namna wanaTajati
walivyoshiriki kwa asilimia kubwa katika shughuli za mazishi ikiwa ni kushusha mwili wa marehemu kwenye
gari, kupeleka ndani kuutoa nje wakati
wa ibada na kuupeleka makaburini kasha kushusha kaburini na kuzika.
“ Niwashukuru sana wenzangu kwa sapoti mliyonipa sina cha zaidi zaidi ya kuwashukuru moyo
mlioonesha ni mkubwa sana” alisema Felix
Mwakyembe.
No comments:
Post a Comment