Dereva akipata Huduma
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida
dereva wa gari la Taqwa lililopata ajali
Mei 11 mwaka huu na kujeruhi watu 15 amesema ametelekezwa na tajiri wake akiwa
amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari
alikolazwa Dereva huyo David Mtachi, Wadi namba moja katika hospitali ya Rufaa
ya Mbeya alisema wakati ajali ikitokea yeye alikuwa amepokewa Iringa lakini cha ajabu tangu afikishwe Rufaa
hakuna alichopata kutoka kwa tajiri wake.
Alisema dereva aliyempokea gari
kutoka Iringa ni Salum Seleman ambaye alipata ajali eneo la Mswisi Wilaya ya
Mbarali Mkoani Hapa na kujeruhi abiria 15 akiwemo yeye.
Alisema tangu kipindi cha ajali
tajiri wake hajawahi kutuma hata salamu za pole wala kumtembelea hospitalini
anakoendelea na matibabuambapo alitumia muda huo kuwashukuru madaktari wa
Hospitali ya Rufaa kwa kumhudumia vizuri.
Gari hiyo mali ya kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 791
BZR aina ya Nissan iliyogongana na magari mengine.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Mbeya,
Nyigesa Wankyo alithibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kuongeza kuwa Gari hilo
lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Salumu Selemani (45) mkazi wa Dar
es salaam kisha kuligonga gari lenye namba za usajili T 778 CAN Isuzu ftr
likiendeshwa na dereva aitwaye Edwin Luyenga (40) na kisha kugonga kwa nyuma
gari T 565 CVB likiwa na tela lenye namba T 836 BBC aina ya Man lililokuwa
limeharibika na kuegeshwa.
Kaimu Kamanda alisema ajali hiyo
ilitokea majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Kapyo, kata ya Mahongole,
Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya
Mbeya/Njombe.
Aliwataja majeruhi katika
ajali hiyo ni wanaume tisa (09) na wanawake sita (06) walifahamika kwa majina
ya Pamat Umuyu (41) Mkongo, Salumu Rashidi (29) mkazi wa Dsm, Juma Rajabu (34)
mkazi wa Zanzibar, Anna Misikita (36) Mkongo, David Mtachi (43) mkazi wa
Dsm, Groli Amani (41) mkazi wa Dsm, Kelvin Jordan (39) mkazi wa Dsm, Waziri
Omary (35) mkazi wa Dsm na Mchembe George (35) mkazi wa Mwanza.
Wengine ni Lika Ilunga (47) mkazi
wa Congo, Majariwa Ramadhani (51) mkazi wa Kagera, Adela Mutomba (46) mkazi wa
Congo, Mudy Abdallah (43) mkazi Bukoba na Nasoro mkazi wa Tanga, majeruhi mmoja
mwanamke ametibiwa na kuruhusiwa na wengine 14 wamelazwa hospitali ya rufaa
Mbeya.
Aliongeza kuwa chanzo cha ajali ni
mwendo kasi wa dereva wa basi ambaye amekamatwa ambapo pia ametoa wito kwa
madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kufuata
sheria,kanuni na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza
kuepukika.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment