KAMATI ya ushauri ya Mkoa wa Mbeya (RCC)
imepitia na kupitisha mapendekezo ya Halmashauri za Mkoa huo ya kugawa majimbo
na mengine kubadili majimbo ya uchaguzi.
Akifafanua katika kikao hicho kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini Mbeya, Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kikao hicho kimekubaliana na baadhi ya
mapendekezo na mengine kuyakataa.
Kandoro alisema mapendekezo hayo yamezingatia
vigezo vilivyotolewa ambavyo ni idadi ya watu katika jimbo na hali ya
Kijografia ambayo inamuwia vigumu Mbunge mmoja kuwafikia wananchi wake
kwakati ikiwa ni pamoja na mawasiliano.
Aliyataja majimbo waliyokubaliana kuyagawa kuwa
ni pamoja na Jimbo la Mbozi Magharibi linalogawanywa kupata majimbo ya Momba na
Tunduma, Mbozi Mashariki inkuwa na majimbo ya Vwawa na Mbozi.
Kandoro alisema jimbo lingine lililopitishwa
kugawanywa ni Jimbo la Mbeya vijijini linalokuwa na Jimbo la Santilya na Mbeya
vijijini na kufafanua kuwa Jimbo hilo linakosa kigezo cha idadi ya watu lakini
kutokana na hali ya Jografia na mawasiliano ni vigumu kuongozwa na Mbunge
mmoja.
Aliongeza kuwa Majimbo mengine yamebadilishwa
majina kutokanana mapendekezo ya Halmashauri ambayo ni Jimbo la Rungwe
Mashariki kuwa Jimbo la Busokelo na Jimbo la Rungwe Magharibi kuwa jimbo la
Rungwe.
Alisema Majimbo mengine yaliyopendekezwa na
halmashari ni pamoja na Halmshauri ya Jiji la Mbeya lakini wazo lao
limekataliwa kutokana na kukosa vigezo ambavyo ni kuwa na idadi ndogo ya watu,
kuwa na mawasiliano mazuri na ukubwa wa eneo linalofikia kilomita za mraba 214.
Aliongeza kuwa vigezo vingine vinavyoifanya
Halmashauri ya jiji kushindwa kugawanywa ni kutokana na kutokuwa na changamoto
nyingi zinazowakabili wananchi, muingiliano wa mamlaka kwa majimbo mawili kuwa
chini ya Halmashauri moja.
Alisema Jimbo la Kyela pia limekosa kigezo cha
kugawanywa hivyo litaendelea kubaki jimbo moja kama ilivyokuwa awali likiungana
na majimbo ya Ileje, Lupa,Songwe na Mbarali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment