Mwenyekiti wa baraza la wazee wa Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, Frank Phiri akitoa tamko kwa waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa baraza la wazee wa Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, Frank Phiri akiwa na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa baraza la wazee wa Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, Frank Phiri akiwa na waandishi wa habari.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa baraza la wazee.
WAJUMBE
wa Baraza la wazee wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi
wameingilia kati mgogoro uliodumu ndani ya kanisa hilo kwa muda wa miaka
miwili.
Mgogoro huo uliodumu kwa miaka miwili umekuwa ukiwahusisha Askofu wa Jimbo hilo, Alinikisa Cheyo na Mwenyekiti
wa Jimbo Mchungaji Nosigwe Buya pamoja
na Halmashauri kuu ya kanisa.
Kutokana na kudumu kwa mgogoro
huo ndani ya kanisa, Baraza la wazee wa Moravian Jimbo la kusini magharibi
limetoa tamko la kumlaani Askofu Alinikisa Cheyo na Halmashauri kuu kwa
kushindwa kutatua na kumaliza mgogoro huo.
Akisoma tamko hilo kwa vyombo
vya habari, Mwenyekiti wa Mabaraza ya Wazee, Frank Phiri, alisema kwa
kipindi hicho cha miaka miwiliimeonekana Wajumbe wa Halmashauri kuu na Askofu
Alinikisa Cheyo wanauendeleza mgogoro huo na hawataki maridhiano ndani ya
kanisa.
Phiri alisema kitendo hicho
kinalitia aibu Kanisa ambapo wakristo kupitia mabaraza ya wazee kutoka shirika
mbali mbali za jimbo la Kusini magharibi hawakuchoka kutafuta amani ndani ya
kanisa ambapo walikutana Mei 2, mwaka huu na kupitia mwenendo wa mgogoro huo.
Alisema baada ya kupitia
mwenendo mzima baraza hilo liliazimia na kukubaliana kumtambua Mchungaji
Nosigwe Buya kama Mwenyekiti halali wa Kanisa la Moravian Jimbo la kusini
magharibi tangu alivyochaguliwa Oktoba 2012.
Alisema makubaliano mengine
Baraza linamuagiza Mwenyekiti Buya kuitisha Sinodi ya pekee haraka
iwezekanavyo, wajumbe wa Halmashauri kuu wanatakiwa kusimamia Katiba ya
Moravian na kutopeleka masuala ya kanisa mahakamani.
Aliongeza kuwa Baraza la wazee
pia linawatambua Wachungaji wote waliosimamishwa kutoa huduma kutokana na
mgogoro huo na kuwataka kuendelea na kazi yao ya kuhubiri.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa
kutokana na ukiukaji wa maksudi na wazi wazi wa katiba ya kanisa la Moravian
Tanzania, Baraza limeiagiza Halmasahuri kuu ya Jimbo kutomzuia kwa namna yoyote
kufanya kazi kama Mwenyekiti Mchungaji Nosigwe Buya.
“ Kwa kuwa Mwenyekiti ameagizwa
kumaliza mgogoro kwa njia ya sinodi, hatutegemei tena kusikia malumbano au
kumzuia kufanya kazi ya Mungu kama tulivyo watuma na bwana alivyowaweka katika
shamba lake, tunaomba wachungaji na wakristo tuendelee kuiombea Sinodi iliyo
mbele yetu ili kuleta amani, upendo, umoja na mshikamano wa kanisa kama Mwanzo”
alisisitiza Mchungaji huyo.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment