Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, May 7, 2015

VIJANA 181 WA CCM MBEYA VIJIJINI WAPATIWA MAFUNZO.

 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine
 Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbeya vijijini Japhet Siulanga aitoa taarifa ya mafunzo.
 Mwenyekiti wa UVCCM, Wilaya ya Mbeya vijijini Msafiri Mwashambwa akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na washiriki wa mafunzo.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mbeya Aman Kajuna akizungumza na vijana waliomaliza mafunzo.
 Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mbeya vijijini, Ipyana Seme akizungumza jambo.
Mwenyekiti wa Vijana akipongezana na Mwenyekiti wa Chama
  Mwenyekiti akimpa mmoja wa washiriki wa mafunzo kadi ya Chama cha Mapinduzi.
Mkufunzi wa Green Guard, Nyirenda akihamasisha washiriki wa mafunzo kuimba nyimbo za Chama.
Vijana waliomaliza mafunzo wakiwa ukumbini wakati wa kufunga kambi.

VIJANA 181 wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya vijijini wamepatiwa mafunzo maalum ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna amewataka Vijana kuwaepuka wanasiasa hususani wagombea wanaoeneza na kufanya kampeni za ubaguzi wa dini na ukabila kuwa utawagawa na kupelekea mpasuko ndani ya chama.
 
Kajuna alisema Vijana wakiendelea kufumbia macho tabia hizo zitaleta mgawanyiko mkubwa miongoni mwa jamii na hatimaye kusababisha machafuko.
 
Alisema vijana wakiendelea kuyafumbia macho maneno ya kubaguana wataendelea kushuhudia majimbo yanavyochukuliwa na vyama vya upinzani kutokanana kugawanywa kwa wanachama na wagombea.
 
Alisema mafunzo waliyoyapata yawasaidie kukishauri Chama hususani mtu nayepaswa kusimamishwa kwa ajili ya kugombea Ubunge na udiwani ili awe chaguo la wananchi na sio kuchaguliwa na viongozi kwa maslahi yao.
 
Alisema kitendo cha viongozi kuwachagulia wananchi bila matakwa yao jambo ambalo linasababisha kupelekewa mgombea ambaye sio chaguo lao na hivyo kuamua kupoteza kura kwa kumpigia mtu mwingine ambaye hakutegemewa.
 
Akijibia kauli hiyo, Mwenyekiti wa C CM Wilaya ya Mbeya vijijini Ipyana Seme alisema katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao atahakikisha anawaita wote wakaotangaza nia ya kugombea ubunge ili kuwaonya kuacha vitendo vya kuhubiri siasa za kibaguzi.
 
Awali akitoa taarifa ya mafunzo kwa mgeni rasmi, Katibu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Mbeya vijijini, Japheti Siulanga, ambaye pia alikuwa Mkuu wa Kambi alisema mafunzo yalianza Aprili 29 hadi Mei 5 mwaka huu ambapo vijana watano watano kutoka kila kata walipaswa kuhudhuria.
 
Alisema matarajio yalikuwa kupata vijana 256 lakini waliohudhuria walikuwa 181 ambao walipata mafunzo katika mada tisa  ambazo zilitolewa na viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa.
 
Alizitaja mada hizo kuwa ni pamoja na Nini majukumu ya vijana kuelekea uchaguzi mkuu, majukumu ya vijana baada ya uchaguzi mkuu, umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la mpiga kura na kuipigia kura ya ndiyo katika inayopendekezwa mada zilizofundishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya.
 
Mada zingine ni Mahusiano ya Umoja wa Vijana wa CCM na Chama mada iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Lackson Mwanjale, Mahusiano ya Umoja wa Vijana wa CCM na Dola ambayo ni Serikali iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya, Anderson Kabenga.
 
Zingine ni nini maana ya neon Escrow mada iliyotolewa na Kada wa Chama Samson Nswila, Mada ya Uchumi iliyotolewa na Kamanda wa Vijana Wilaya ya Mbeya Oran Njeza na Mada ya usimamizi wa uchaguzi pamoja na mawakala iliyotolewa na Katibu wa Chama wa Wilaya Mary Mary Kalisinja.
 Na Mbeya yetu

No comments: