Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akitoa hutuba katika harambee ya kanisa la GMCL
Mchungaji Aquina Mhanze akisoma risala ya kanisa mbele ya mgeni rasmi
Nabii Mpanji akihubiri kabla ya kuanza kwa harambee
Naibu Waziri pamoja na meza kuu wakicheza moja ya nyimbo zilizoimbwa kanisani hapo.
Waumini wakifuatilia Ibada ya Harambee kanisani hapo
NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu
Nchemba(Mb) jana aliwaongoza mamia ya waumini Kanisa la GMCL lililopo Ilomba
jijini Mbeya kukusanya fedha zaidi ya
shilingi Milioni 53 katika harambee ya kuchangia miradi ya Kanisa hilo.
Katika Harambee hiyo ambayo
Mwigulu Nchemba alikuwa mgeni rasmi zilipatikana fedha taslimu shilingi Milioni
2.7 na Ahadi shilingi Milion 50,235,000 na
kufanya jumla kufikia shilingi Milioni 53,017000.
Awali wakisoma risala ya Kanisa
mbele ya mgeni rasmi iliyosomwa na Mchungaji Aquina Mhanze, walisema Kanisa
limekuwa likiendesha ibada zake kwa njia ya vyombo vya habari ili kuwafikia waumini
wengi jambo ambalo linagharimu fedha nyingi za kuendeshea zoezi hilo.
Mchungaji Mhanze alisema huduma
hiyo ilianza mwaka 2012 ambapo zaidi ya shilingi Milioni 40 zilikuwa zikitumika
fedha ambazo zilikuwa ni michango ya waumini ambazo kila muumini alilazimika
kuchanga shilingi 5000 hadi 10,000 kwa mwezi ili kufanikisha huduma hiyo.
Alisema baada ya kuona zoezi
hilo linakuwa gumu wakaunda kamati maalumu ambayo ilipewa jukumu la kuhakikisha
wanakuwa na kituo cha Redio, ambapo zilihitajika Shilingi Bilioni Moja
kuanzisha redio hiyo lakini fedha zilizopatikana hadi Mwaka jana zilikua
Shilingi Milioni 150 ambazo zilifanikisha kuanzisha kituo cha Redio cha GMCL
fm.
Alisema pamoja na kufanikiwa
kuanzisha redio hiyo bado inakabiliwa na changamoto ambazo zimelazimu kuitishwa
kwa harambee hiyo ambazo kukosekana kwa ubora wa matangazo yanayotokana na
ukosefu wa Standby Jenereta ili kukabiliana na umeme unapokatika, vyuma vya
kurefushia mnara na Transmita vitu vinavyogharimu Shilingi Milioni 50.
Alisema Changamoto nyingine ni
ukosefu wa ofisi kwa ajili ya kuendeshea redio hiyo inayogharimu shilingi
Milioni 150 hivyo kufanya jumla ya shilingi Milioni 200 kuhitajika kwa ajili ya
kukamilishia miradi ya Kanisa hilo.
akijibu Risala hiyo Mwigulu
Nchemba alilipongeza Kanisa kwa juhudi za kuongeza miradi kuwa jambo hilo
linaelekea kuwakomboa Watanzania na kuwajenga katika imani ili wawe na hofu ya
kumjua Mungu.
Alisema mbali na kuwaongoza
waumini kuchangisha shilingi Milioni 53,017,000 pia atakuwa Miongoni mwa
Wanakamati ili kuhakikisha malengo ya kukamilisha miradi hiyo inafanikiwa ikiwa
ni pamoja na kuwaunganisha na marafiki zake wanaoishi nje ya Mkoa wa Mbeya.
“Niongezeni kwenye kamati yenu
lengo sio kumaliza na kukamilisha ratiba ya leo bali ni kutimiza yaliyokusudiwa, mmelenga kuniita mimi kwani
kila mnachoongelea ni Injili, Kanisa na Miradi hilo lina baraka sana na laiti
Watanzania wangejua umuhimu wa injili haya yanayolikumba Taifa yasingetokea”
Alisem Naibu Waziri.
Na Mbeya yetu
TANGAZO
TANGAZO MPYA KABISA: CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) KAMPASI YA MBEYA. , NAFASI ZA MASOMO – SEPTEMBA 2015/2016 WAHI SASA
No comments:
Post a Comment