Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, May 13, 2015

ANKAL ISSA MICHUZI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA TONE MULTIMEDIA GROUP (TONE HOUSE) NA KUONA STUDIO YA TONE RADIO-TZAnkal akiwa na Mkurugenzi Fredy Njeje katika jengo la Tone House ambamo kuna mambo kibao ikiwa ni pamoja na studio za  Tone Radio-TZ lililopo Mwenge jijini Dar es salaam. Hapa ndipo nyumbani pa libeneke la Blog za Mikoa kama vile Mbeya Yetu, Lindi Yetu, Mwanza Yetu na kadhalika. Hawa vijana pia ni wanachama waanzilishi wa Tanzania Bloggers Network (TBN) ambayo inazidi kukua siku hadi siku...  Haya si maneno yetu ni Maneno ya Ankali Mwenyewe.

Ankal Issa Michuzi Kutoka Michuzi Media Group ambao ni Wamiliki wa Michuzi Blog  pamoja na Michuzi TV   Jana alitembelea Makao makuu ya Tone Multimedia Group (Tone House) na kujionea Shughuli mbalimbali ambazo wanazifanya, na baadhi yake amezitaja hapo juu, Pia alipata nafasi ya Kuona Studio za Kurushia matangazo ya Online ya Tone Radio-Tz 

Hii ilikuwa ni Ziara Muhimu kwa sababu tulijifunza mengi na Kubadilishana uzoefu. Asante kututembelea
No comments: