Mwenyekiti wa Redcross Mkoa wa Mbeya, Ulimboka Mwakilili akizungumza na timu muda mfupi kabla hazijaingia uwanjani.
Timu zikisalimiana.
Wachezaji wa Timu ya Ghana wakiwa katika picha ya pamoja
Wachezaji wa Timu ya Mabatini wakiwa katika picha ya pamoja
Timu zikiwa uwanjani zikitimua vumbi.
Wachezaji wa timu ya mabatini wakishangilia baada ya kuibuka mabingwa
TIMU ya Kombaini ya Kata ya
Mabatini ilifanikiwa kuibuka kidedea katika fainali za Kombe la Red Cross 2015
zilizofanyika Mei 8, mwaka huu katika viwanja vya shule ya Msingi RuanzaNzovwe
baada ya kuifunga Goli Moja kwa bila timu ya Kombaini ya Kata ya Ghana.
Mchezaji Daniel William
aliiwezesha timu yake ya Mabatini kupata goli la ushindi dakika ya 30 ya
kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa timu ya
Ghana.
Kutokana na ushindi huo Timu ya
Mabatini ilijinyakulia Kikombe, Jezi seti moja 15 na Mpira mmoja huku timu ya
Ghana ambao ni mshindi wa Pili akijinyakulia Seti moja ya Jezi 15 na Mpira
mmoja na Mshindi wa tatu ilikuwa Kata ya Ilomba walioambulia Jezi Seti moja.
Akizungumza wakati wa kufunga
mashindano hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu(Redcross)Mkoa wa Mbeya,
Ulimboka Mwakilili alisema ligi hiyo hufanyika kila mwaka ikiwa ni maadhimisho
ya msalaba mwekundu duniani.
Alisema Ligi iyo ilianza kutimia
vumbi Aprili 27, Mwaka huu kwa kuzikutanisha timu kutoka katika Kata 12 ambazo
ni Mabatini, Nzovwe, Iyela,Ghana, Isyesye, Ruanda, Ilemi, Uyole, Mwakibete,
Iyunga, Ilomba na Isanga.
Alisema lengo la michuano hiyo
ni kutoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Mbeya pamoja na kuinua vipaji ambapo
katika mashindano hayo watachaguliwa vijana 25 watakaounda timu ya Mkoa
itakayofanya ziara katika mikoa ya Arusha na Morogoro.
Aliongeza kuwa mbali na ziara
hiyo pia watachambuliwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 ambao wataweza
kutembelea Nchi za Nje ambazo ni wanachama wa Redcross kwa kucheza nazo michozo
kadhaa.
Na Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment