Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 18, 2015

HOT NEWS: MWIGULU NCHEMBA ATAKIWA ATANGAZE KUGOMBEA URAIS NA KUACHA WOGA‏

 Nabii Mpanji akimuombea Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Waumini wa Kanisa la GMCL wakifuatilia Ibada

MKURUGENZI wa Kituo cha Redio cha GMCL fm na Mwasisi wa Kanisa la GMCL lililopo Ilomba Jijini Mbeya, Nabii Mpanji,amemtaka Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba kuacha uoga wa kutangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.
 
Nabii huyo aliyasema hayo  alipokuwa akihubiri katika ibada ya Harambee ya kuchangia miradi ya Kanisa ambapo Naibu Waziri alialikwa kama mgeni rasmi, na kuongeza kuwa asiwe na wasi wasi wa kutangaza nia kutokana na kuwa na watu wengi nyuma yake.


 
Alisema yeye kama Nabii ameoneshwa kuwa kuna mafuta ya uongozi kwa Mwigulu Nchemba hivyo asiogope kutangaza nia kwa kuwahofia wazee kwani Taifa kwa sasa linahitaji kijana mzalengo na mchapa kazi ambaye ataweza kukusanya kodi na kusimamaia Watanzania wenye vipato vya chini.
 
“Wapo wanaonibeza kuwa mimi ni Nabii wa Uongo lakini katika watu nilioneshwa wenye nia ya kwenda Ikulu na wewe umo hivyo usiwaogope wazee,Sema leo hapa watu wakusikie, Maandiko yanasema Fahari ya Wazee ni Mvi zao na fahari ya vijana ni nguvu sisi tunahitaji vijana” alisisitiza Nabii Mpanji.
 
Aliongeza kuwa mara nyingi viongozi wa Serikali wamekuwa wakiwataka viongozi wa dini kuliombea Taifa pamoja na uchaguzi Mkuu ujao lakini hakuna anayerudi kuchukua majibu juu ya maombi hayo kama Mungu amejibu nini kuhusiana na uchaguzi huo.
 
“Nimesimama hapa kwa niaba ya Serikali ya Mbinguni na ninakupa mafuta ambayo mtu yoyote atakayejaribu kuchafua nyota yake atachafuka mwenyewe kwani kinachohitajika ni Pesa mfukoni, Yesu moyoni na akili Kichwani” alisema Nabii huyo huku akishangiliwa na waumini wake.
 
Aliongeza kuwa Taifa linahitaji mabadiliko kwa kumpata kiongozi mzalendo mwenye uchungu na mapato ya Watanzania na kuongeza kuwa Kanisa la GMCL liko tayari kumchangia fedha za kuchukulia fomu ya kugombea urais.
 
“Neno linalotoka kinywani kwa Nabii ni sheria wako maherode wengi  hao wasikukatishe tamaa waswahili wanasema kaza buti” alimalizia Nabii Mpanji.
 
Kwa upande wake Mwigulu Nchemba alijibu kauli ya Nabii kwa kunukuu maneno machache kutoka Kitabu kitakatifu cha Biblia akisema“Heri mtu Yule asiye na mashaka na mimi” Kodi zitakusanywa na zitatumika vizuri.
 
“Nawashukuru Watanzania wenye imani na mimi bado kitambo kidogo ili taratibu za Kichama zikamilike hivyo nitasema kwa sasa tusubiri tuko ukingoni mwa mto Jordani tunakaribia kuvuka” alisisitiza Nchemba huku waumini wakimshangilia kwa kumuita Rais.
 
Na Mbeya yetu
                                                                                                          

No comments: