Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bi. Theo Ntara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Kyela (watatu kutoka kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt.
Hamza Kabelwa (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na
washiriki wa warsha inayohusu uboreshaji wa huduma za hali ya hewa
katika maeneo ya Ziwa Nyasa kwa sekta ya wakulima na wafugaji, wavuvi na
wasafirishaji, tarehe 14 Mei 2015 katika hotel ya Kyela Resort-Mbeya.
Mamlaka
ya Hali ya Hewa kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani
kupitia mpango wa utoaji wa huduma za hali ya hewa wa GFCS yaani “Global
Framework for Climate Services” imezindua rasmi huduma ya kutoa
taarifa za hali ya hewa hususan tahadhari na utabiri mahususi kwa
watumiaji wa ziwa nyasa. Taarifa hizo zitasamabazwa kupitia vyombo mali
mbali vya habari ikiwemo redio za kijamii. Huduma hiyo ilizinduliwa
rasmi tarehe 11 Mei 2015 huko Kyela mkoani Mbeya na Mheshimiwa Mkuu wa
Wilaya ya Kyela Dkt. Thea Ntara aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Katika
kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu TMA wameandaa warsha ya
“UBORESHAJI NA UAINISHAJI WA MAHITAJI YA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA
MAENEO YA ZIWA NYASA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI, WAVUVI NA WASAFIRISHAJI’’
iliyofanyika katika hotel ya Kyela Resort jijini Mbeya. Akiongea kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bi. Thea Ntara alisema ‘Hivi karibuni
tumeshuhudia matukio ya mvua ya mawe, mafuriko na radi katika baadhi ya
maeneo ya mkoa wa Mbeya, hali hii imesababisha madhara makubwa ya
kijamii na kiuchumi.
Nimatumaini
yangu kuwa taarifa zinazopatikana kutoka kwa wananchi na wataalam
mbalimbali kupitia semina hii zitaiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa
kuboresha taarifa zake kwa umma na kuwawezesha watalaam kutoa ushauri
stahiki unaozingatia taarifa za hali ya hewa’. Alizungumza hayo wakati
akifungua rasmi warsha ya wadau wa hali ya hewa wanaotumia ziwa nyasa
iliyowajumuisha wasafirishaji, wakulima, wavuvi, wafugaji, Ofisi ya
Bandari, SUMATRA,usalama, Maafa, maliasili na vyombo vya habari.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi katika hotuba yake
iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Utabiri TMA Dkt. Hamza Kabelwa alisema
‘Katika kuhakikisha TMA inazidi kuziboresha huduma zake, wataalam wa TMA
wameweza kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyela ili kupata
uelewa zaidi wa majanga yanayoikumbuka wilaya hiyo na namna gani ya
kuweza kufanyia kazi’.
‘TMA
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari
imejikita katika kuhakikisha jamii inapata taarifa za hali ya hewa kwa
wakati hususan kunapokuwa na vipindi vya matukio ya hali mbaya ya hewa
kama vile mvua kubwa, ukame, upepo mkali, mawimbi makubwa n.k kwa lengo
la kuisaidia jamii kuchukua tahadhari mapema ili kupunguza athari
zinazoweza kusababishwa na matukio hayo hivyo kuchangia katika kuokoa
maisha ya watu na mali zao’ alisema Dkt. Kijazi.
IMETOLEWA NA MONICA MUTONI AFISA HABARI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment