Mwezeshaji wa mkufunzi kutoka TAPBDS, Sizya Puya akiendesha mafunzo kwa wajasiliamali kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini yaliyofanyika jijini Mbeya.
Mwezeshaji wa mkufunzi kutoka TAPBDS, Sizya Puya (aliyesimama mbele)akiendesha mafunzo kwa wajasiliamali kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini yaliyofanyika jijini Mbeya
Wajasiliamali wakiwa katika mafunzo
Mfanyabiashara wa Hotel ya Mbeya Peak, Lusajo Mwakoba akielezea matarajio yake
Mfanyabiashara wa Kuchomelea, Stela Mwashalinda akieleza matarajio yake baada ya mafunzo kutoka safari lager wezeshwa
Mkufunzi wa wajasiliamali akiendelea kutoa mada.
Mwezeshaji akitoa maelekezo kwa washiriki wa mafunzo
WAJASILIAMALI 12 kutoka mikoa ya Kanda ya nyanda za juu kusini
wamepatiwa mafunzo juu ya kusimamia na kuendesha biashara zao.
Mafunzo hayo yameratibiwa na Kampuni ya bia Tanzania(TBL) kupitia
shindano la Safari lager wezeshwa yanayofanyika kwa siku tano katika hoteli ya
Peter Safari iliyopo Ilomba jijini Mbeya, mafunzo ambayo yatatolewa kuanzia
Aprili 13 hadi Aprili 17, mwaka huu.
Akizungumza katika mafunzo hayo, mkufunzi mwezeshaji wa usimamizi
na uendeshaji wa biashara, Sizya Puya kutoka kampuni ya TAPBDS, alisema lengo
la mafunzo ni kuwawezesha wafanyabiashara waliondani ya biashara zao kuacha
kuendesha kimazoea bila tija.
Alisema Kampuni ya Bia ya TBL imekuwa na mchakato wa kuwainua
wajasiliamali wadogo kwa kuwaongezea mitaji katika biashara zao kupitia
shindano la Safari lager wezeshwa ambapo mjasiliamali hujaza fomu maalumu kisha
huchujwa na kuwapata waliokidhi vigezo na masharti.
Aliongeza kuwa mchakato wa kuwapata wafanyabiashara hao ulianza
mwezi Februari mwaka huu ambapo wafanyabiashara waliojitokeza walikuwa 29 ambao
walichujwa baada ya kutembelea katika maeneo yao ya biashara na kubakia 12
watakaopatiwa mafunzo kisha vifaa walivyoomba kwa ajili ya biashara zao.
Puya alisema wajasiliamali waliofanikiwa kupita kwenye mchujo
wanatarajia kukabidhiwa vifaa vyao mwishoni mwa mwezi huu, vitu ambavyo
vimeombwa na mfanyabiashara mwenyewe ili kuongeza nguvu kwenye mtaji wake.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo waliipongeza
kampuni ya bia (TBL) kwa kuanzisha mchakato ambao huwainua wafanyabiashara
ambao mara nyingi wanashindwa kuendesha biashara zao kutokana na kukosa mitaji
ya kutosha kumudu mahitaji mbali mbali.
Mfanyabiashara Lusajo Mwakoba anayeendesha biashara ya Hoteli
inayojulikana kwa jina la Mbeya Peak alisema aliingia kwenye shindano ili aweze
kuboresha huduma ya chakula kwa ajili ya wateja wake pamoja na kuanzisha
upikaji wa vyakula kwenye masherehe.
Alisema amelazimika kuboresha sehemu ya chakula akiamini kuwa
kitakuwa kichocheo cha wateja kufika kupata huduma za vinywaji na malazi ambao
anatarajia kuongeza wapishi wazuri pamoja na vitendea kazi.
Naye Stellah Mwashalinda mfanyabiashara wa kuchomelea alisema
matarajio yake ni kuongeza vitendea kazi kwani mara nyingi alikuwa akikosa
baadhi ya kazi kutokana na ukosefu wa mashine kwani wateja wake wengi wanatoka
nje ya eneo lake la kazi.
.
No comments:
Post a Comment