Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Winfrida Igogo akitoa mada katika mafunzo ya wanafunzi wanaosoma masomo ya manunuzi na ugavi katika Chuo cha TIA Mbeya.
Mwezeshaji, Juvenal Joseph, akitoa mada katika mafunzo ya wanafunzi wanaosoma masomo ya manunuzi na ugavi katika Chuo cha TIA Mbeya
Katibu Mtendaji wa Umoja wa wanataaluma wa masomo ya ununuzi na ugavi wa TIA (PSA-TIA) kutoka makao makuu Dar es salaam,Joseph Mwashimaha, akitoa salamu.
Mlezi wa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) Kampas ya Mbeya, Bwana. Mgaya akizungumza jambo katika mafunzo ya wanafunzi wa manunuzi na ugavi.
Mwenyekiti wa PSA-TIA, Tawi la Mbeya, Aiman Awadh akiongoza mkutano wa mafunzo.
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa TIA Kampas ya Mbeya, Gabriel Luhanga akizungumza jambo katika mafunzo ya wanafunzi wa manunuzi na ugavi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiuliza maswali kutoka kwa wawezeshaji.
Wanafunzi ambao wanasoma masomo ya manunuzi na ugavi wakifuatilia mafunzo yaliyotolewa na Bodi ya manunuzi na ugavi katika chuo cha uhasibu Mbeya.
BODI ya manunuzi na ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo kwa wanafunzi
waosoma masomo ya manunuzi na ugavi katika chuo cha uhasibu(TIA) Mbeya.
Katika mafunzo hayo wito ulitolewa kwa Taasisi binafsi na
serikali kuepuka kutoa ajira katika sekta ya manunuzi na ugavi kwa watu ambao
hawana taaluma hiyo wala kusajiliwa na Bodi ya PSPTB.
Wito huo ulitolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya
Manunuzi na ugavi(PSPTB), Winfrida Igogo, alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa
Wanafunzi wa taasisi ya Uhasibu kampasi ya Mbeya ambao ni wanachama wa Umoja wa
wanataaluma wa manunuzi na Ugavi(PSA-TIA) wakati wa mafunzo yaliyofanyika
katika ukumbi wa TIA Mbeya.
Igogo alisema hairuhusiwi kwa mtu yoyote kufanya kazi za
manunuzi na ugavi bila kuwa na utalaam pamoja na kusajiriwa na bodi kwani
kufanya hivyo ni kosa kisheria jambo ambalo adhabu inamkumba pia mwajiri.
Alisema lengo la kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya
manunuzi na ugavi(procurement & supply)ni kuwajengea uwezo na kuwahamasisha
juu ya taratibu wanazopaswa kuzifuata wakiwa kazini kuhusiana na manunuzi na
ugavi.
Aliongeza kuwa lengo lingine ni kuwakumbusha wanataaluma hao
kujisajili na bodi mara baada ya kuhitimu masomo yao jambo ambalo litasaidia
upatikanaji wa ajira haraka tofauti na wasio sajiliwa ambao hukaa muda mrefu
bila ajira kutokana na kukosa kipengere cha uzoefu.
Alisema Bodi ipo kwa mujibu wa sheria ambapo hivi sasa ipo
kwenye mchakato wa kupitia kila taasisi kukagua kama walioajiriwa wanasifa za
manunuzi na ugavi ikiwa pia kupitia matangazo mbali mbali ya ajira kama vigezo
vinavyowekwa vipo kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake Mwezeshaji mwingine katika mafunzo hayo, Juvenal
Joseph, alisema ni vema wataalamu wa manunuzi na ugavi wakazingatia sheria kwa
kuepuka mikataba inayoweza kuwaingiza matatizoni.
Alisema wataalam wa manunuzi na ugavi wanapaswa kujua kuwa kila
mikataba ni makubaliano lakini sio kila makubaliano yanaweza kuwa mikataba
hivyo wajiepushe kutumbukia katika rushwa kwa kukiuka taratibu za manunuzi na
ugavi.
Naye Mlezi wa Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya
Mbeya aliyejitambulisha kwa jina moja la Mgaya alisema Wanafunzi wanaosomea
masomo ya manunuzi na ugavi wanapaswa kuwa na nidhamu katika masomo yao ili
kuepuka kuwa maafisa wav yeti.
Aidha Mwalimu wa Somo la Manunuzi na ugavi chuoni hapo,
aliyejitambulisha kwa jina la Gasibila aliishukuru bodi kwa kuendesha mafunzo
hayo na kuongeza kuwa jambo hilo litasaidia kuzalisha wahitimu wenye taaluma na
kupata watumishi waliotukuka.
Aliongeza kuwa waalimu na watumishi katika fani ya manunuzi na
ugavi wanategemea maelekezo kutoka miongozo kutoka bodi kwa kuwa wao ndiyo dira
ya utumishi mzuri nchini.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment