Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, April 27, 2015

KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA AKUNJUA MAKUCHA, AWAJIA JUU KAMATI YA SIASA WANAOWANIA UBUNGE.   Kiongozi wa Green guard akitoa salamu za heshima kwa Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda alivyofanya ziara mkoani Mbeya.
   Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda, akivalishwa skafu baada ya kuwasili katika viwanja vya ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
   Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda pamoja na viongozi wengine wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano.
   Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda, akihutubia Umoja wa vijana Wilaya ya Mbeya mjini.
   Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna akizungumza katika mkutano wa vijana wilaya ya Mbeya mjini.
    Mjumbe wa Mkutano mkuu kupitia Wilaya ya Mbeya mjini(MNEC), Sambwee Shitambala akiwasalimia vijana.
   Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, akiwasalimia vijana katika mkutano wao.
         Baadhi ya vijana wakiwa wamefurika katika mkutano huo.

          
  WAJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mbeya mjini wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wametakiwa kuachia nafasi zao ndani ya Chama endapo watakuwa wakitaka kuwania ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao.
   
  Rai hiyo ilitolewa  na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM)Taifa, Sixtus Mapunda alipokuwa akizungumza na Umoja wa Vijana wa Wilaya ya Mbeya mjini katika mkutano wao wa kawaida wa kila mwisho wa Mwezi uliofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mbeya.
   
  Mapunda alisema kitendo cha Wajumbe wote wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mbeya mjini kutangaza nia ya kutaka kugombea ubunge ndiyo sababu iliyopelekea Chama hicho kupoteza jimbo la Mbeya mjini katika uchaguzi uliopita na kuchukuliwa na Chadema.
   
  Alisema wajumbe wa Kamati ya Siasa ndiyo wanaopaswa kumpigia kampeni mgombea wa Ubunge lakini kila mtu anapokuwa akitaka nafasi hiyo analeta mgawanyiko ndani ya Chama jambo linalopelekea kuwepo kwa mivutano na hatimaye kupoteza jimbo kwa mara ya pili.
   
  Aliongeza kuwa Umoja wa Vijana hauko tayari kuona mvutano wa kisiasa ukiendelea katika Jimbo la Mbeya mjini kutokana na kila mjumbe kutaka yeye ateuliwe kugombea ubunge hali inayopelekea kuamua kuwa kila mtu akose na sio kuungana mkono.
   
  “ Nasema kwa macho makavu bila kupepesa macho wala kumung’unya maneno, sisi Vijana hatuko tayari kuingilia mivutano ya ubunge,haiwezekani Kamati nzima ya siasa mnataka ubunge nani atampigia kampeni mwenzie, Hivyo basi tamko la Umoja wa vijana ni kwamba anayetaka ubunge ajiondoe kwenye kamati ya Siasa tutakaa wenyewe” alisisitiza Katibu huyo.
   
  Alisema kwa hali ilivyosasa Vijana hawatamvumilia kiongozi mkubwa anayetaka kuua Chama kwa lengo la kutaka uongozi na kuwafanya Vijana kuwa mbuzi wa kafara bali ataanza kuwajibishwa yeye kabla ya kuharibu utaratibu wa Chama.
   
  “Tumechoka kuwa mbuzi wa kafara katika vita ya wakubwa kutaka uongozi, hivyo basi safari hii hatukosi wote kama mnavyofanya kila uchaguzi bali tutaanza na nyie kwanza, pia hatuko tayari kusubiri kuona mtu anataka kutoboa mtumbwi ili tuzame kwa sasa tutamzamisha yeye kwanza” alisema Mapunda.
   
  Aidha katika hatua nyingine Mapunda alisema kuanzia Sasa vijana wa Mbeya mjini wanaajenda moja ya kuhakikisha Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi(SUGU) wa Chadema anang’olewa katika nafasi hiyo kwa gharama yoyote kwa madai kuwa anafanya siasa za hovyo za kuwagawa wananchi.
   
  Alisema lengo la kumuondoa Sugu katika ubunge ni kutokana na kueneza chuki na viurugu kwa wakazi wa Mbeya hata akiwa Bungeni jambo linalochangia kuchelewa kwa shughuli za maendeleo katika Jiji la Mbeyalicha ya Serikali kujitahidi katika kila hali.
   
  “Kuanzia sasa tunatengeneza operesheni kabambe ya Ng’oa Sugu ambayo itahubiriwa kila kona kila eneo la Jiji la Mbeya hadi atakapoondoka madarakani kwani ni aibu kujitambulisha eti mbunge wangu ni sugu maana hata sisi tuliomchagua tunaonekana wote akili zetu kama Sugu” alisema Mapunda.
    Na Mbeya yetu

  1 comment:

  Anonymous said...

  Bati hilo kutu tupu CCM, badilisheni hilo bati la office za CCM.