Afisa uhusiano wa Kajuna cup 2015, Rashid Abdalah akizungumza na waandishi wa habari.
Afisa uhusiano, Rashid Abdalah akiwa na Mratibu wa mashindano ya Kajuna Cup 2015, David Nyembe katika mkutano na waandishi wa habari.
Afisa uhusiano, Rashid Abdalah akiwa na Mratibu wa mashindano ya Kajuna Cup 2015, David Nyembe katika mkutano na waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika mkutano wa maandalizi ya ligi ya Kajuna cup 2015.
TIMU zaidi ya 50 zinatarajia
kupambana katika kuwania kitita cha shilingi Milioni moja katika ligi ya mpira wa miguu Jiji la Mbeya itakayoanza
kutimua vumbi Mei mosi mwaka huu katika viwanja tofauti.
Akizungumza na vyombo vya
habari katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Sokoine, Afisa uhusiano wa
Ligi hiyo, Rashid Abdalah, alisema ligi hiyo itajilikana kwa jina la Kajuna cup
2015 kutokana na kufadhiliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Mkoa wa Mbeya,
Aman Kajuna.
Alisema lengo la kuanzisha ligi
hiyo ni kuibua vipaji kwa wakazi wa Mbeya ili baadaye ipatikane timu nyingine
ambayo inaweza kuungana na timu za Tanzania Prison na Mbeya city katika ligi
kuu Tanzania bara.
Abdalah alisema ligi hiyo
itaendeshwa kwa mtindo wa mtoano ambayo itachezwa katika viwanja vinne tofauti
ambavyo ni uwanja wa Uyole, Shule ya Msingi Mwege, shule ya msingi Ruandanzovwe
na uwanja wa Shule ya msingi Mbata.
Alisema timu zitakazoshiriki
ligi hiyo zitanunua fomu maalumu ambayo itauzwa kwa shilingi 30,000, fomu
ambazo zitaambatanishwa na kanuni mbali mbali zitakazosaidia kuendesha ligi
pasipokuwa na misuguano yoyote.
Alizitaja zawadi ambazo
washindi watazipata kuwa ni kila kiwanja kitatoa msindi mmoja ambaye atapata
zawadi lakini Mshindi wa jumla wa kwanza atajipatia shilingi Milioni moja,
Mshindi wa pili shilingi laki tano na timu yenye nidhamu shilingi laki mbili.
No comments:
Post a Comment