- Kama unahisi Gari lako haliko sawa ukipita hapa unaweza ukaliacha kabisa
- Barabara imechafuka kwa makorongo
- Haina Unafuu wowote ule.
Hiki ni Kipande kuanzia eneo la Jamatini
Ukiwa hapa unaweza kusema hii Barabara imesingiziwa hakuna kasheshe huko mbeleni
Ukianza kushuka kiduchu tuu kama haupo makini utavaana na hili Shimo hapa
Na kama haitoshi ukisogea kiasi tuu hapa utacheza sindimba kidogo, kwa wenzetu wenye magari madogo hii huwa ni shidaah!
Hali ya Barabara inazidi kuwa tata.... Hapa una macho tazama mwenyewe
Hapa ni Heka heka za kutafuta unafuu
Sasa hapa unapita wapi dereva?
Hapa Hali inazidi kuwa mbaya zaidi sasa Makorongo mashimo kila kitu kipo hapa Ni hatari kwa kweli
Huku Chini ndio kabisa unaweza ukakata tamaa...
Tochi yetu imemulika tuu kama unavyo ona
Je hapa kwa hali hii inamaana hapaonekani?
Ikumbukwe haya ni maeneo tafauti kakipande ka Jamatini mpaka Rift Valley
Hakuna unafuu hapa ndio mwisho unapoingia barabara ya kutoka mjini mpaka Mafiati ... Napo ndio majanga kabisaaaa......
Sasa tunaomba kuuliza je Hii barabara itaangaliwa lini? ni swali tunalowaachia wahusika wetu mana ni muda mrefu sana papo tuu!
Bado tutaendelea kumulika maajabu zaidi ya haya ... Stay tuned
Picha na Mbeya yetu
1 comment:
Nawapongeza blog ya Mbeya yetu. Mwanzoni nilisema ninyi ndo mutakaofanikisha maendeleo mkoani Mbeya. Kidogo mulirudi nyuma. Tunataka Mbeya iwe kama jiji la New York Marekani. Sehemu zote na vitongoji vyake viwe na lami na hii inawezekana kabisa endapo viongozi wetu wataamua. Pesa ipo sana ya maendeleo ya mkoa, nafikiri ni mipango na uamuzi. Hongera sana blog ya Mbeya yetu.
Post a Comment