Mtafiti wa maswala ya kijamii kutoka Mtandaowa jinsia Tanzania(TGNP), Dinah Nkya,akitoa mada katika semina ya waandishi wa habari kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini.
Afisa uhusiano wa TGNP, Melkizedeck Karol akiendesha mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari.
Waraghibishi kutoka kituo cha maarifa na taarifa cha Tuamke, Nsalaga wakiwa kwenye chumba cha semina baada ya kutoa mambo mbali mbali waliyoyafumbua kutoka vijijini.
Waandishi wa habari wakishiriki semina hiyo.
IMEELEZWA kuwa iwapo wanawake wataendelea kuwa nyuma katika kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo Urais bado changamoto zilizopo katika jamii zitaendelea kuwatesa wanawake nchini.
Kauli hiyo imetolewa na ofisa mawasiliamo wa mtandeao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Melikizedeck Karol wakati akitoa mada ya ushiriki wa wanawake kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015 wakati wa mafunzo ya siku mbili ya wanahabari mikoa ya nyanda za juu kusini. Yaliyofanyika jijini Mbeya.
Alisema kuwa usawa katika nafasi za uongozi wa kutaka kuwa na asilimia 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume ni lazima utimie katika uchaguzi huu kwa wanawake kuanza kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali zikiwemo za juu kama Urais ,ubunge na udiwani .
Hata hivyo Ofisa huyo alisema kwamba mwaka 2005 kuwa akidi nzima ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni wabunge 357 kwa mujibu wa katiba hata hivyo viti maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6 vilivyogawanywa miongoni mwa vyama vya siasa kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi kati ya viti 239 vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni wanawake 21 tu sawa na asilimia 8.8 ndio walipewa viti vya kuchaguliwa bungeni.
Alisema ili kuwepo na usawa hakuna budi kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ikiwemo urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
"Hivi wataka kusema hakuna mwanamke katika nchi hii ambae anaweza kuongeza nchini kama Rais na kama wapo kwanini hawajitokezi kugombea nafasi za juu kama Urais .....lazima wanawake wachangamkie nafasi hiyo "
Alisema kwa mwaka 2005 kuwa akidi nzima ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni wabunge 357 kwa mujibu wa katiba hata hivyo viti maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6 vilivyogawanywa miongoni mwa vyama vya siasa kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi kati ya viti 239 vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni wanawake 21 tu sawa na asilimia 8.8 ndio walipewa viti vya kuchaguliwa bungeni.
Huku idadi ya madiwani wa kuchaguliwa asilimia 4 na wenyeviti wa vijiji ni asilimia 2 wakati wenyeviti wa vitongoji ni asilimia 3 .
Hivyo alisema ni wajibu kwa vyombo vya habari na wanawabari nchini kuendelea kuhamasisha makundi ya vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi katika nafasi za udiwani ,ubunge na Urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Na Mbeya yetu Blog
No comments:
Post a Comment