Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, April 2, 2015

HATARI MTAA WA MPAKA SOKOMATOLA, DIWANI UPO? JE MKANDARASI WA JIJI UMEKIONA KIFUSI HIKI CHENYE ZAIDI YA MIEZI MINNE BILA KUREKEBISHA BARABARA HII? SHUHUDIA

  • Wakazi wa eneo Hili walalamika kuwa sasa ni zaidi ya Miezi minne hakuna hata dalili za kuijenga Barabara hii 
  • Sasa eneo hili limekuwa Pori rasmi ambapo hakuna hata pakupitisha Bajaji , Pikipiki na Hata Baiskeri kukatiza kwa shida
  • Mmoja wa kiongozi wa Serikali za mtaa huu anaishi njia hii hii lakini sasa hatujui kama anaina haya au lah
  • Huu ni Mtaa wa Maendeleo ambapo Kuna kituo kikubwa cha Afya cha Kiwanja Mpaka sasa hivi kweli hapa inakuwaje?
  • Ungana nasi kushuhudia msije mkazania tunawaonea....

Huu ni mtaa wa mpaka uliopo Sokomatola ambapo kwa kuangalia tuu hapa katika kibao utagundua kuwa ni eneo ambalo limesha sahaulika kitambo sana.



Tazama hiki kifusi kwa makini sana utagundua ni kweli kipo hapa kwa zaidi ya miezi minne lakini wanakiangalia tuu, au zamu yao mpaka sasa haijafika?

Cha kusikitisha zaidi tazama hiki kifusi ambapo njia hii ndiyo ingeweza ikawa inafikika kwa haraka zaidi katika kituo cha afya kikubwa kabisa cha Kiwanja mpaka , sasa hapa Gari zinapitaje? Msomaji wetu na wewe Jiulize.
Hapa picha halisi inaonesha wazi kuwa Kifusi hiki kimeanzia barabarani kabisa kwenda chini Njia nzima imezibwa sasa je hii ni haki au Mkandarasi wa Jiji anaweza kuwa na majibu hapa kwa nini mpaka sasa ukarabati huu haujafanyika.
Ukiangalia kwa umakini kabisa utaona kuwa hapa ni ishara tosha inayotutambulisha kuwa eneo hili kuna kiongozi anapatikana.


Sasa Mwenye macho haambiwi tazama Wote mtatusaidia kweli hii ni sawa? Je Diwani wa kata hii ya Maendeleo upo? na Pia wananchi au wakazi wa mtaa huu mmewasikia kiliochao? Na vipi kuhusu Jiji Mkandarasi unaonaje hii? 

Ni kweli tumeona mmeonesha moyo mmeweka kifusi ... hatuna pingamizi lakini sasa kifusi kinaishi zaidi ya miezi minne tena au ndio kihifadhio eneo hili?

Basi sawa hii Sintofahamu Tunawaachia wasomaji wetu, Tunakaribisha maoni yenu juu ya hili.


Kumbuka Tochi ya Mbeya yetu inaendelea kumulikia Jiji kona zote.. Endelea fuatilia... Maendeleo ni Muhimu Jiji liwe jiji Kweli.

Na Mbeya yetu.

No comments: