Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 2, 2015

WANANCHI WA KATA YA MASOKO WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA HAWATAKI PIGA KURA ZA MAONI YA KATIBA MPYA NA UCHAGUZI MKUU KUTOKANA NA KUTOKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI WA MASOKO

PRF. PETER MSOLWA MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MAJI KILIMO NA UFUGAJI AKIONGEA NA WANANCHI WA KATA YA MASOKO WALIOJITOKEZA KUMSIKILIZA , MWENYEKITI NA KAMATI YAKE WALIPATA WAKATI MGUMU WA KUPOKELEWA KATIKA MRADI WA MAJI WA MASOKO KUTOKANA NA JINSI MRADI UNAVYOTEKELZWA KWA KUSUASUA 

PRF. PETER MSOLWA MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MAJI KILIMO NA UFUGAJI AKIONGEA NA WANANCHI WA KATA YA MASOKO WALIOJITOKEZA KUMSIKILIZA ,(HAWAPO PICHANI ) MWENYEKITI NA KAMATI YAKE WALIPATA WAKATI MGUMU WA KUPOKELEWA KATIKA MRADI WA MAJI WA MASOKO KUTOKANA NA JINSI MRADI UNAVYOTEKELZWA KWA KUSUASUA

WA PILI KULIA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE EZEKIA MWAKOTA AKIONGA NA WANANCHI KATIKA MOJA YA MIRADI ILIYOTEMBELEWA NA KAMATI 

CHRISTINA MSENGI MHANDISI WA MAJI WILAYA YA RUNGWE AKIELEZA JINSI CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI WAKATI WA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI WILAYANI RUNGWE HUKU KELO IKIWA NI MRADI WA MAJI WA MASOKO MRADI AMBAO UMESIMAMA HUKU WANANCHI WAKIHITAJI MAJI PASIPO NA MAFANIKIO TANGU MWAKA 2012 HADI SASA MAJI HAKUNA 

PICHA YA PAMOJA KAMATI YA BUNGE MKUU WA WILAYA YA RUNGWE NA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE KABLA YA KUTEMBELEA MIRADI YA MAJI


Wananchi wa kata ya masoko wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya wamesema hawatopiga kura ya maoni ya rasim ya katiba na kwa  kuipigia kura ccm kwa kushindwa kutekeleza mradi wa maji wa masoko ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2012 mpaka sasa mwaka 2015 haujakamilika.

Akiongea kwa niaba ya wananchi  diwani wa kata ya kisiba bwana Samweli  Mwakyusa kupitia chama cha Mapinduzi  amesema kwamba mradi huo wa maji umeshusha  hadhi ya chama cha CCM  kwa kuwa mradiwa maji umegubikwa na utekelezaji mbovu na siasa zinazopelekea viongozi wa serikali na chama kutokuwa waaminifu katika kutekeleza mradi huo na mpaka sasa wananchi kukosa maji.

 Wakiongea wananchi mbele ya kamati ya maji kilimo na mifugo iliyongozwa na mwenyekiti wa kamati Prf. Peter Kusolwa kiwemo mbunge wa Rungwe magharibi Prf. David Mwakyusa mzaliwa wa  kata hiyo ya masoko ambako mradi wa maji unatekelezwa, wananchi  wanashangaa kuona hata mbunge wao hajawasaidia huku mkuu wa wilaya Crispin Meela akifanya ziara nyingi zisizo na mafanikio katika mradi huo wa masoko .

 Kamati ya Bunge ya maji kilimo na mifugo ikiongozwa na mwenye kiti wa kamati  prf. Peter kusolwa  na kuongozana na  mbunge wa  Rungwe magharibi na kupokelewa  na mkuu wa wilaya, makamu wa halmashauri ya  Rungwe na busokelo na viongozi wa maji mkoa wa Mbeya na Tukuyu.  imetembelea na kukagua miradi ya maji wirayani Rungwe, miradi iliyotembelewa ni mradi wa kijiji cha itete na Kapugi na mradi wa masoko.

Kabla ya kukagua miradi hiyo mkuu wa wilaya alikabidhi ripoti za miradi hiyo na kuelezea changamoto walizokumbana nazo kuwa ni kukosa wataaram wa maji, na madeni ambayo yamepelekea kutomalizika kwa baadhi ya miradi. Hivyo alishauri serikali kuanzisha wakara wa miradi ya maji vijijini kwani hii itawasaidia kupambana na changamoto zinazowakabiri na  ameitaka wizara ya maji kuiga mbinu zinazofanywa na wizara ya miundo mbinu ili kukamilisha miradi mikubwa ambayo haijakamilika.

Nae makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Rungwe diwani Ezekiel mwakota amesema kwamba tatizo ni mtiririko wa fedha na ndio chanzo cha kutomalizika kwa miradi mbalimbali. Na mradi uliokwama ni mradi wa masoko  na ni kutokana na kukosa fedha za kuendelezea mradi huo.

Wakazi wa kijiji cha Itete na Kapugi wameipongeza serikari kwa kufanikisha mradi  wa maji wa Kapugi na Itete na wameomba kuongezewa mpira utakoakuwa unatoa maji kutoka chanzo kwenda  kijiji cha  Itete na Kapugi kwani bomba la mpira lililopopo  linatumika na vijiji vitatu kikiwemo kijiji cha kyimo na halmashauri tayari inampango wa kutoa mpira wa nchi tatu utakao peleka maji katika  vijij vilivyoomba bomba hilo.

Kamati ya maji kilimo na ufugaji  imedai kushughurikia matatizo hayo na kuwashauri wananchi kuunda kamati  ya maji itakayosimamia miradi hiyo na kutunza mazingira  ili kutunza vyanzo vya maji  kwani vitawakomboa wasitembee umbali mrefu wakitafuta maji  na wamewaasa  kuchemsha maji ya kunywa kuepukana magonjwa ya matumbo.
TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA
  

No comments: