Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, February 20, 2015

HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA IMEANZA KUSAMBAZA NAKALA ZA KATIBA PENDEKEZWA KWA WANANCHI.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro akizungumza na wananchi wa Chunya waliofika katika uzinduzi wa zoezi la kusambaza nakala za katiba mpya inayopendekezwa kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro akiwasomea wananchi wake moja ya vipengere vilivyomo ndani ya Katiba inayopendekezwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri yaWilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli, akitoa taarifa juu ya nakala zitakazosambazwa kwa wananchi wa Wilaya ya Chunya


Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro, akiwagawia baadhi ya wananchi nakala za Katiba inayopendekezwa.Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi la kuzindua ugawaji wa Katiba wakifuatilia kwa makini.


Moja ya nakala za Katiba mpya inayopendekezwa.HALMASHAURI ya Wilaya ya Chunya imeanza zoezi la kuzisambaza nakala za Katiba mpya inayopendekezwa kwa Wananchi wake ili waweze kuisoma na hatimaye kuipigia kura Aprili 30, mwaka huu.

Akizungumza na wananchi katika hafla ya kuzindua zoezi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro, iliyofanyika  kwenye stendi ya mabasi, alisema Wilaya imepokea nakala 10200 ambazo zitasambazwa katika kata zote 34 ambapo kila Kata itapata nakala 380 kwa ajili ya kuwasambazia Wananchi.

Kinawiro aliwataka Maafisa Watendaji wa Vijiji na Kata kuhakikisha nakala hizo zinasambazwa kwa wakati katika maeneo yote yanayohusika ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kuisoma kabla muda wa kuipigia kura haujafika.

Alisema kunakuwa na tabia kwa baadhi ya Watendaji wasio waaminifu ambao watataka kutumia urasimi wakati wa ugawaji wa katiba pendekezwa jambo litakalochangia wananchi wengi kuzikosa ikiwa ni pamoja na wao kukaa nazo maofisini na wengine kujaribu kuuza, jambo alilosema halijakubalika na atakayebainika kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa ili nakala hizo za Katiba ziweze kuwafikia wananchi wengi na kwa wakati ni bora zoezi hilo likafanyika kwa siku nne huku sekta mbali mbali na makundi maalumu yakipewa kipaumbele zikiwemo idara za Serikali, Maktaba, ofisi za Vijiji na Kata na Mashuleni.

Alisema kwa wazazi ambao hawajui kusoma na wanapenda kusomewa ni bora Nakala hizo pia zikawafikia Wanafunzi ambao wataweza kuwa msaada kwa hao watu baada ya wao kuzisoma na kuweza kuwasaidia kuwaelimisha pale ambapo wataona kuna umuhimu wa kuelezwa.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli, alisema Nakala za Katiba hizo zimegawiwa kulingana na uhitaji na kuongeza kuwa kutokana na ukubwa wa Wilaya na mchanganyiko wa watu waliopo idadi hiyo haitoshi kuwafikia wote.

Alisema kwa mujibu wa sensa ya Mwaka 2012 Wilaya ya Chunya ina watu zaidi ya laki 3 ambao ni mchanganyiko wa wakulima, wafugaji, wachimba madini, viongozi wa dini mbali mbali, watumishi wa taasisi za serikali na taasisi binafsi ambazo zote zinapaswa kupewa kipaumbele cha kupata nakala za Katiba inayopendekezwa.

Mwisho.
Na  Mbeya yetu

No comments: