Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, February 22, 2015

WAZIRI MKUU PINDA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MBEYA.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abass Kandoro





WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda,anatarajia
kufanya ziara ya ya kikazi kwa siku nane mkoani Mbeya.



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abass Kandoro,alisema jana(Feb 20) kuwa Pinda
anatarajiwa kuwasili mkoani hapa Februari 23 majira ya saa kumi jioni na
akiwa mkoani hapa atatembelea halmashauri saba.



Kandoro alizitaja halmashauri zitakazotembelewa na waziri mkuu kuwa ni
halmashauri ya wilaya ya Mbeya,jiji la Mbeya,Kyela,Busokelo,Rungwe,Chunya
na Mbozi.



Alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
inayotekelezwa na serikali,halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo
katika mkoa wa Mbeya.



Mkuu huyo wa mkoa alisema katika ziara yake,Pinda atakagua,kuweka mawe ya
msingi na kuzindua miradi latika sekta ya Elimu,Afya,ujenzi,barabara,kilimo
na umwagiliaji,maji,masoko na hifadhi ya chakula.



Alisema pia waziri mkuu akiwa katika halmashauri hizo atahutubia wananchi
katika mikutano ya hadhara hivyo aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi
kwenye mikutano hiyo sambamba na maeneo mengine atakayopitia.

Na Mbeya yetu

1 comment:

Anonymous said...

Mheshimiwa Kandoro, tunaomba ujenzi wa barabara kutoka Iyunga, upande wa Iyunga Secondary School iwekwe lami. Ile barabara inaweza kuwa msaada mkubwa wa kupunguza msongamano wa magari toka Iyunga mpaka Iwambi or mbalizi. Ni Ombi tu kwa Mheshimiwa RC. Pia barabara za kuelekea viwandani vya Pepsi Tanesco na kuelekea kiwanda cha bia ni kero sana wakati wa mvua sijui munalionaje hilo nalo. Tunataka Jiji la Mbeya lipambwe kwa lami tupu kabla hujahamishwa Mheshimiwa Kandoro. Ombi hili naomba likufikie wewe mwenyewe.